Hadithi : Shemeji Monica – Sehemu ya 5

Hadithi : Shemeji Monica – Sehemu ya 5

0

Siku hiyo James alifundisha hiyo basi tu, lakini akili yake yote ilikuwa kwa Julieth, alitamani muda ufike mapema ili aende kukutana naye na kulianzisha rasmi penzi lao.


Baada ya kipindi hakupoteza muda, akamuaga Sir Mdharuba na safari ya kuelekea nyumbani kwa kina Julieth ikaanza. Ndani ya dakika kumi tu akawa amefika kwani alikwenda kwa usafiri wa bodaboda, akapokelewa na mlinzi wa getini na kuruhusiwa kuingia ndani ambapo alimkuta Julieth akiwa amekaa mzee ambaye kwa umri wake James alihisi kuwa alikuwa ni baba yake, na kweli alikuwa sahihi.

?karibu mwalimu? alikaribisha mzee yule akiupamba uso wake kwa tabasamu la ukarimi ambalo lilimfanya James nae kulitoa lakwake bila hiyari yake, ?naitwa Mr. Priscus, mimi ni baba yake Julieth? alijitambulisha mzee yule ambaye alisimama na kumpa mkono wake James. ?bila shaka wewe ni mwalimu James, Julieth amenieleza sana kuhusu wewe, na amefurahia sana huduma yako? alielezea mzee Priscus akimkaribisha James kwenye kochi ambapoa alikaa na maongezi ya hapa na pale yakaanza. James akagundua kuwa baba yake Julieth alikuwa ni balozi wa nchi hii kwenye nchi moja ya Ulaya, hivyo hakuwa mkaaji wa muda mrefu hapa nchini, alikuwa amekuja kuisaimia tu familia yake. Baada ya maongezi ya hapa na pale ukafika wakati wa James kufanya ambacho kilikuwa kimempeleka pale, na Julieth akamtaka waelekee chumbani kwake ambapo somo lingefanyika siku hiyo kwani hakutaka kumsumbua baba yake ambaye alikuwa akiangalia TV pale sebuleni, James akatii na kuongozana na Julieth mpaka chumbani kwake.

Aina 8 za Vyakula vinavyopunguza nguvu za Kiume


Kilikuwa chumba kikubwa ambacho kilikuwa na vitu vya thamani sana ndani yake, mpangilio wa chumba pia ulikuwa wa kuvutia sana. Hatua kama nne kutoka kilipokuwa kitanda kulikuwa na meza mbayo ilikuwa na vifaa mbalimbali vya kusomea ambavyo vilikuwa vimepangwa vizuri, pia kulikuwa na viti viwili ambavyo bila shaka vilikuwa kwa matumizi sambamba na meza ile na vifaa vya kusomea ambavyo vilikuwepo mezani.

James na Julieth wakakalia viti vile na kipindi kikaanza, lakini James aligundua kuwa Julieth hakuwa kwenye kipindi siku hiyo, muda mwingi aliutumia kumuangalia usoni baadala ya kuangalia kilichokuwa kinafundishwa, lakini James akajifanya kama alikuwa halioni hilo, hakuwa tayari kuanzisha chochote kutokana na uoga kama ilivyokuwa kawaida yake, kipindi kikaendelea. Baada ya dakika kama tano tu uzalendo ukamshinda Julieth ?kwanini uliamua kunichunia baada ya kukueleza hisia zangu?? alihoji Julieth akimkazia macho James.

Sababu ya Mwanaume kulala baada ya kupiga Bao wakati wa Sex

?hapana sikukuchunia, kifurushi changu kiliisha na nilikuwa nyumbani tayari na muda ulikuwa umeenda, nikashindwa kupata vocha? alijitetea James. ?mmh! Sio kweli, mbona hata baada ya kukucha hukufanya chochote?? aliuliza Julieth kwa sauti ya kudeka. ?hebu tumalizie kusoma kwanza kisha tutaongea vizuri? alishawishi James lakini ndo kama aliua kipindi kwani Julieth alihama kutoka mezani mapaka kitandani huku akisema ?aah! Mi hata sijisikii kusoma leo, tuongee tu?.

James hakuwa na namna zaidi ya kutoka pale kwenye meza na kumfuata Julieth pale kitandani ?nilijua lazima jioni nitakuja na tutaongea, sikuona ulazima wa kukutafuta asubuhi, kama nilikuudhi nisamehe basi mpenzi? alianza ‘kujibebisha’ James akijaibu kuifanya sauti yake kuwa romantic huku akimshikashika Julieth maeneo ya nyuma ya shingo yake kumfariji, hakujua kama Julieth alikuwa na udhaifu mkubwa kwenye maeneo hayo, alimuona tu akianza kuwa mpole na kukakamaza mwili kama askari amekutana na mkubwa wake wa kazi. James akagundua haraka kuwa huko anakoelekea atazua matatizo, akaacha haraka sana, lakini alikuwa amechelewa, alikuwa ‘ameliamsha dude’ tayari, akashangaa kumuona Julieth akiamka pale kitandani kimyakimya na kwenda kufunga mlango vizuri kwa funguo, kisha akarudi na kukaa pembeni yake huku akimuangalia kwa macho ambayo yalieleza kila ambacho kilikuwa kikiendelea ndani ya moyo wake. ?Julieth hapa ni nyumbani kwenu na wazazi wako wapo, sio vizur…?

Alijaribu kuongea maneno ya kukwepa Jukumu lile ambalo aliona kama lilikuwa hatarishi lakini kabla hajamalizia maneno yake tayari kinywa cha Julieth kilikuwa kimekutana na chakwake huku Julieth akimkumbatia kwanguvu. James akajikuta hana maamuzi tena, kwani akili yake ilimruka, akawa anafikiria kwa kutumia mnara wake ambao haukutaka kusikia habari nyingine yoyote ila kula tunda lile ambalo lilikuwa limejipeleka lenyewe kwa mlaji likiwa limeiva na kutengeneza rangi ya kuvutia macho ya mlaji.

Akiendelea na lile zoezi la kunyonyana ambalo alilianzisha Julieth, James akawa wa anapandisha juu sketi ya Julieth kisha akakutana na kufuli lake ambalo hata hakuwa amejua rangi yake kwani macho yake yalikuwa yamefumbwa yakifaidi utamu uliokuwa ukiendelea na mkono ambao ulikuwa na uwezo wa kufanya kazi ya ziada haukuwa na macho, akaishusha kufuli ile mpaka maeneo ya mapajani na akaona inatosha kwani mkao wao haukuweza haukumruhusu kwenda zaidi ya hapo, akapeleka kidole kirefu zaidi ya mkono wake wa kulia mpaka chumvini kwa Julieth lakini akakutana na hali ambayo hakuitarajia, njia haikuwa inatosheleza kupita kama alivyodhani, akajaribu kuongeza muda kidogo, Julieth akaruka na kuchomoka kwenye ‘denda’ lililokuwa likiendelea ?mwenzio sijawahi kufanya, leo ndo mara ya kwanza? alisema Julieth kwa sauti ya kimahaba na macho yake yalikuwa yamelegea sana. Habari hii ilikuwa tata kwa James, hata ‘mzuka’ wa kuendelea na chezo lile ukakata, yeye mwenyewe alikuwa mwanafunzi tu kwenye mambo haya na hakuwa amewahi kumbikiri mwanamke kabla, ataanzaje leo katika mzingira yale hatarishi? ?sasa kama wewe bado ni bikra, tusifanyie hili jambo hapa, tunaweza kukamatwa? alisema Jamesa ambaye aligundua anaweza kumwambia chochote Julieth na akamuamini kwani hakuwa akijua chochote. ?hakuna mtu ataingia chumbani kwangu, kwanza nimefunga mlango? alisema Julieth, akaweka kituo kidogo na kumtizama James machoni, ?mpango wangu ulikuwa kutomjua mwanaume mpaka niolewe ila baada ya kukutana na wewe nataka kufanya, ‘so please’? alisema Julieth kwa hisia kali sana, alionekana kulitaka sana penzi la James. ?ahsante sana kwa kuamua kunipa mimi hiyo zawadi, ila nakwambia sio ‘good idea’ kufanyia hapa, especially kwa hii mara ya kwanza, kama kweli unanipenda naomba unielewe,vinginevyo unaweza kuniweka matatizoni? alijieleza James. Maneno yale ya mwisho yakaonekana kumshawishi Julieth ambaye alikubaliana na matakwa ya James, ?basi hug me please? aliseme Julieth macho yake yakionekana kulengwa na machozi akimtaka James amkumbatie jambo ambalo James alilitekeleza bila ubishi, wakakumbatiana kwa muda, mwisho wakajilaza kitandani wakiwa wamekumbaliana. ?nakupenda sana Julieth na kama Mungu akiruhusu nitapenda uwe mke wangu?

James alijitahidi kusema maneno matamu ili kumfariji mpenzi wake huyu mpya ambaye alionekana wazi kutoridhishwa na maamuzi yaliyofanyika. ?nakupenda pia James, ni muda mrefu sana sijapenda kama ambavyo nimekupenda wewe? alisema Julieth na akashindwa kuyazuia machozi yake. ?no no no, don’t cry baby? alisema James huku akimfuta machozi Julieth na kumkubatia tena.


James alikaa na Julieth mule chumbani kwake mpaka akavusha hata muda ambao kipindi kilipaswa kuisha. Julieth alimuelezea juu ya mpenzi wake aliyepita ambaye ndiye pekee aliyewahi kuwanaye, alikuwa ni kijana mwenye asili ya Kiarabu ambaye alikutana naye wakati akisoma O’level, shule zao zilijenga mazoea ya kutembeleana na kufanya mitihani ya pamoja ili kujipima uwezo. Julieth na kijana huyo ambaye alimtaja kama Farid walishindwana kwa sababu kuu mbili, moja ikiwa tofauti ya dini zao lakini ya pili ilikuwa kushindwa kwa Farid kutekeleza malengo ya Julieth ambaye hakutaka kumpa uhondo mpaka ndoa, mwisho Farid alijaribu kumbaka Julieth baada ya kuona kupewa penzi kistaarabu ni jambo ambalo halikuwepo. ?yani alinitamkia kabisa kuwa hawezi kufanya upumbavu wa kusubiri mpaka ndoa wakati aliona kabisa ndoa kati yetu haikuwepo kutokana na tofauti zetu za dini? alielezea Julieth story ambayo hakupenda kuielezea kwa watu kwani aliona ni ya aibu pia ilikuwa ikimsababishia kulia. ?pole sana, hakufanikiwa lakini?? aliuliza James ambaye alikuwa ameguswa sana na story ile. ?hapana, rafiki yake ambaye tulikuwa kwao wakati hayo yakiendelea alinihurumia, akafanikiwa kuzuia rafiki yake nami nikapata nafasi ya kukimbia? alielezea Julieth huku akifuta machozi. ?wewe ni mwanaume wa tofauti sana, kwani wanaume hutaka mapenzi tu kwa mwanamke lakini nimegundua kwako hicho sio kipaombele? alisema Julieth na kumfanya James ahisi kuwa huenda hiki kilichomkuta huko nyuma ndicho kilisababisha akataka sana kumpa penzi akidhani kama hatompa huenda akamkosa kama alivyomkosa Farid. ?kufanya tedo ni kitu cha ziada tu kama unampenda mtu kwa dhati, kitu cha kwanza ni kuhakikisha anaendelea kuwa wako kwa gharama yoyote, mimi niko tayari kusubiri mpaka mpaka ndoa, wala sitokuwa na lalamoko lolote, alisema James ili kumtoa wasiwasi mpenzi wake huyo. ?no, nimechagua mwenyewe kufanya na wewe, usininyime tafadhali? alisema Julieth.


Jamani mko hai humo ndani?? ilikuwa sauti ya mama yake Julieth akiuliza huku akigonga mlango. Muda ulikuwa umeenda sana James na Julieth wakiwa wamejifungia mule ndani. Walishtuka wakaona kitasa cha mlango kikinyongwa kama mtu aliyeko nje alitaka kuufungua mlango ule, ?mmmh! Mbona mmejifungia?? alihoji mama yake Julieth kwa wasiwasi.
****************************************
……………………………………Usikose sehemu ya 6

Kupata mwendelezo wa Hadithi HII mpaka sehemu ya 9 Ingia Hapa kwenye App yetu

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY