Je Kakolanya kaenda Shinyanga leo? Yanga wafunguka haya

Je Kakolanya kaenda Shinyanga leo? Yanga wafunguka haya

0

Je Kakolanya kaenda Shinyanga leo? Yanga wafunguka haya

Leo washabiki na wapenzi wa Yanga waliingiwa na hofu kubwa baada ya taarifa za Kipa wa Yanga Klaus Kindoki Kufiwa na baba yake mzazi huko nchini Congo.

Kutokana na taarifa hiyo washabiki wengi waliingiwa na Hofu kuelekea mchezo wao dhidi ya Stand United chama la wana kutokana na kukosekana kwa kipa Ramadhan Kabwili ambaye naye ni majeruhi na Kipa aliyepo Hamid watu wengi wameonekana kutokuwa na imani naye kutokana na kutofanya vizuri Mapinduzi Cup.

Baada ya hayo yote zikazuka Taarifa za Kipa Beno Kakolanya kwenda Shinyanga kuungana na Kikosi cha Yanga.

Lakini afisa habari msaidizi wa Yanga Godlisten Andweson Chicharito amekanusha taarifa hizo kwa kusema hakuna kitu kama hiko bali wachezaji waliopo Shinyanga ni walewale 18 waliosafiri jana.

App kwaajili ya Wakubwa Tu, Ona na Jifunze Mengi Hapa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY