Kocha Mwadui apagawa na uwezo wa mchezaji huyu Yanga

Kocha Mwadui apagawa na uwezo wa mchezaji huyu Yanga

0

Kocha Mwadui apagawa na uwezo wa mchezaji huyu Yanga

KOCHA Mkuu wa timu Mwadui FC, Ally Bizimungu, ameweka wazi kwamba anatamani kuwa na wachezaji kama Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Yanga katika kikosi chake.

Akizungumza nasi, Bizimungu, ambaye ni raia wa Rwanda, alisema kikosi kikiwa na wachezaji watano wenye kiwango kama Fei Toto, benchi la ufundi haliwezi kuihofia timu yoyote ambayo watakutana nayo.

“Fei Toto ni mchezaji mwenye uwezo, licha ya umri wake kuwa mdogo lakini ana akili ya mpira, anajua muda gani afanye nini kwa manufaa ya timu, hivi ndivyo inavyotakiwa.

“Nimempenda sana huyu kijana, natamani kuwa na wachezaji wa aina yake, maana ukiwa nao sita hufikirii matokeo hata kama utakutana na timu ngumu,” alisema.

Aidha, Bizimungu alifafanua kuwa bao alilofunga Fei Toto katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita alitumia akili kulingana na mazingira aliyokuwapo.

“Angekuwa mchezaji mwingine asingethubutu kupiga shuti, badala yake angetoa pasi kwa mwenzake, lakini yeye alijiongeza na kuipa bao timu yake, hivi ndivyo mchezaji anavyotakiwa kufanya,” alisema.

Wakati huo huo, kocha huyo ameitangazia vita Azam FC, akitamba kuwa wataondoka na pointi tatu kesho katika mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Alisema amekiandaa vyema kikosi chake kuhakikisha kinaibuka na ushindi ambao anaamini ni muhimu katika vita ya kupambana kujinasua kwenye nafasi za chini.

“Mchezo utakuwa mgumu kutokana na mazingira ya wapinzani wetu yalivyo, lakini ninaamini mbinu tutakazotumia lazima watalala mapema,” alisema.

Jifunze mambo mbali mbali hapa kuhusu Maujanja ya Kimapenzi – Wakubwa Wanafaidi

Bingwa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY