Manula ampoteza kipa wa As Vita kwenye hili

Manula ampoteza kipa wa As Vita kwenye hili

0

Manula ampoteza kipa wa As Vita kwenye hili

MABINGWA watetezi Simba wa Ligi Kuu Bara, Jumamosi watakuwa nchini DR Congo kwenye Uwanja wa Martyrs kumenyana na AS Vita ya DR Congo huku rekodi zikionyesha kwamba mikono ya mlinda mlango wa Simba, Aishi Manula imempoteza mlinda mlango wa AS Vita ya Congo, Nelson Lukong.

Katika michezo mitatu ambayo ni ya hatua ya awali pamoja na mmoja wa hatua ya makundi Manula amempoteza Lukong kwa kufanikiwa kuwa na michezo mingi bila kuruhusu bao.

Manula amefanya hivyo katika mchezo wa kwanza dhidi ya Nkana FC ambapo Simba ilifungwa mabao 2-1, pia katika mchezo wa marudiano Simba ilishinda kwa mabao 3-1 na katika mchezo wa hatua ya makundi Simba walishinda mabao 3-0 na kufanya Manula kufungwa jumla ya mabao matatu kwenye mechi tatu.

Wakati Manula akifanya yake, mlinda mlango wa wapinzani wao, Lukong katika mchezo wao dhidi ya Bantu FC walishinda kwa mabao 4-1 huku ule wa marudiano walitoka kwa sare ya bao 1-1 na mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi wakipoteza mabao 2-0 dhidi ya Al Ahly na kufanya afungwe jumla ya mabao manne, hivyo vita yao itaendelea tena Jumamosi ijayo.

source : Champion

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY