Matokeo ligi kuu TPL 25 January 2019

Matokeo ligi kuu TPL 25 January 2019

0

Ligi kuu soka ya Tanzania bara iliendelea leo kwa mechi mbili kuchezwa ambapo Kulikuwa na mechi mbili ya Kwanza ikiwakutanisha JKT Tanzania walioikaribisha Mtibwa Sugar na ya pili Azam Fc wakiikaribisha Biashara United ya Mara.

Katika mechi iliyochezwa saa kumi kamili alasiri katika uwanja wa meja Jenerali Isamuhyo maafande wa JKT Tanzania wamebanwa na Mtibwa Sugar na kujikuta wakitoka Sare ya bila kufungana.

Na katika mechi ya pili iliyoanza saa moja usiku Azam Fc wameibuka na Ushindi wa Bao 2 kwa 1 dhidi ya Biashara United kutoka Mkoani Mara.

Biashara United ndiyo walioanza kuitikisa Azam Fc kwa kuifunga bao la mapema dakika ya pili ya mchezo bao lililodumu mpaka kipindi cha Kwanza kinamalizika.

Kipindi cha pili Azam Fc walianza kwa kasi na katika dakika ya 46 Salum Aboubakary maarufu kama Sure Boy aliipatia Azam Fc bao la kwanza na la kusawazisha.

Na katika dakika ya 62 Ramadhan Singano “Messi” akaipatia Azam Fc bao la Pili na la Ushindi katika mchezo wa Leo.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY