Matokeo Simba vs Js Saoura leo

Matokeo Simba vs Js Saoura leo

0

Matokeo Simba vs Js Saoura leo

Matokeo ya moja kwa moja kati ya Simba dhidi ya JS Saoura ya nchini Algeria leo mechi ya Hatua ya Makundi klabu bingwa barani Afrika .

Kuanzia saa kumi kamili tutaanza kukupa Live Updates

Mechi Imeanza

Dakika ya 1 Simba wanatengeneza shambulizi na Kupata kona

Inapigwa kona na inazaa kona nyingine

Dakika ya 3 ya mchezo JS Saoura wanapata free kick nje kidogo ya 18 baada ya Juuko kumweka mtu chini

Inapigwa Free kick inawababatiza wachezaji wa Simba

Dakika ya 5

Simba 0 – 0 Js Saoura

Dakika ya 8 Emmanuel Okwi anawachachafya walinzi wa Js Saoura na kisha kumtengea Hassana Dilunga lakini Dilunga anapaisha mpira ule.

Dakika 10

Simba 0 – 0 Js Saoura

Dakika ya 15 kwa mara nyingine Juuko Murshid anamuweka chini mchezaji wa Js Saoura na kuwa Free Kick kuelekea Simba nje kidogo ya 18.

Dakika ya 18 Emmanuel Okwi anafanya kitu kingine Konki anapiga mpira unagonga mwamba na kurejea uwanjani

Dakika 20

Simba 0 – 0 Js Saoura

Dakika ya 22 John Bocco anawatoka vizuri mabeki wa Saoura lakini shuti lake linadakwa na kipa wa Saoura

Dakika ya 25 Simba wanapata kona nyingine ya Mchezo lakini wanashindwa kuitumia vyema

Dakika ya 27 John Bocco anaingia vizuri langoni mwa Js Saoura anapiga pasi ambayo ilimlenga Okwi lakini kipa anaudaka mpira kabla haujamfikia Okwi

Dakika 30

Simba 0 – 0 Js Saoura

Dakika ya 33 Nicolas Gyan anakosa goli la wazi

Dakika ya 34 John Bocco anaonekana kutolewa nje kwenye machela baada ya kuumia na Kagere anainuka kuanza kupasha , washabiki waliopo uwanjani wanalipuka kwa Shangwe

Dakika ya 35 Emmanuel Okwi anapiga shuti nje ya 18 kipa anatoa na kuwa Kona

Dakika ya 37 Meddie Kagere anaingia kuchukua nafasi ya John Bocco aliyeumia

kikosi cha Simba dhidi ya JS Saoura leo

Dakika ya 43 Js Saoura wanapata kona wanashindwa kuitumia

Goaaaaaal Emmanuel Okwi anaipatia Simba bao la Kuongoza, dakika ya 45

HALF TIME

Simba 1 – 0 Js Saoura

KIPINDI CHA PILI

Kipindi cha pili kimeanza

Dakika ya 45 Simba wanapata kona

Goaaaaaaaaal Meddie Kagere anaipatia Simba bao la pili akimalizia kazi nzuri ya Emmanuel Okwi, Walinzi wa Js Saoura walidhani Okwi kaotea wakamuacha na kunyoosha mikono

Simba 2 – 0 Js Saoura

Dakika ya 54 Thomas Ulimwengu anaingia uwanjani kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine wa Saoura

Dakika ya 57 Thomas Ulimwengu anaunganisha mpira kwa kichwa lakini unapaa juu ya Lango

Dakika ya 62 Juuko Murshid anapewa kadi ya njano

Dakika ya 64 Mzamiru Yassin anaingia kuchukua nafasi ya Hassan Dilunga

Goaaaaaal dakika ya 67 Meddie Kagere anaipatia Simba bao la tatu

Simba 3 – 0 Js Saoura

Dakika ya 80

Simba 3 – 0 Js Saoura

Dakika ya 86 Okwi anatoka anaingia Shiza Kichuya

FULL TIME

Simba 3 – 0 Js Saoura

Install app yetu upate Breaking news za Yanga na Simba Bonyeza hapa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY