Matokeo Simba vs Malindi leo Mapinduzi Cup
Matokeo ya Moja kwa moja kati ya Simba dhidi ya Malindi nusu fainali ya pili, Mshindi wa hapa ataungana kucheza fainali na Azam Fc ambao walishinda mechi yao kwa bao 3 kwa 0 dhidi ya KMKM.
Mechi Imeanza
Simba 0 – 0 Malindi
Timu zote zinacheza mpira wa pasi fupi fupi za kuvutia
Dakika ya 13 Simba wanatengeneza nafasi lakini pasi aliyopewa Asante Kwasi na Salamba ili amimine maji inapigwa visivyo na kuwa goal kick
Dakika YA 15 kROSI ya Zana Koulibaly inashindwa kutumiwa vizuri na Adam Salamba anayepiga kichwa kinachopaa juu ya lango
Dakika ya 18 Simba wanapata Free Kick baada ya Dickson Mhilu kuangushwa nje kidogo ya 18.
Inapigwa Free Kick lakini kipa wa Malindi anadaka mpira
Dakika ya 21 Dickson Mhilu anakosa nafasi ya wazi akipenyezewa na Zana mpira unakuwa kona.
Dakika 30
Simba 0 – 0 Malindi
Half time
Simba 0 – 0 Malindi
Kipindi cha pili
Dakika ya 60
Simba 0 – 0 Malindi
Dakika 70 bado timu zote zinapambana kutafuta bao huku milango ikiwa bado migumu
Simba 0 – 0 Malindi
Ddakika ya 80
Simba 0 – 0 Malindi
Zinaongezwa dakika 3 kumaliza pambano
Full time
Simba 0 – 0 Malindi
ZINAFATA PENATI
Jana Coulibaly anapaisha penati , Simba wanakosa penati ya kwanza
Maarifa wa Malindi naye anakosa penati
Yusuph Mlipili anapata penati kwa Simba
Mwarami wa Malindi anakosa penati baada ya Ally Salim kuipangua penati yake
Simba 1 – 0 Malindi
Mi Ibrahim anapata penati kwa Simba
Abdu kassim wa Malindi anapata penati kwa Malindi
Simba 2 – 1 Malindi
Asante Kwasi anapata penati kwa Simba
Ally Chollo anapaisha penati kwa Malindi
Simba 3 – 1 Malindi
Simba wanafuzu fainali sasa watacheza na Azam Fc