Matokeo Yanga vs Biashara United leo 31 January 2019

Matokeo Yanga vs Biashara United leo 31 January 2019

0

Matokeo Yanga vs Biashara United leo 31 January 2019

Matokeo mechi ya Kombe la Shirikisho Azam Sports Federation Cup kati ya Yanga dhidi ya Biashara United

Mechi Imeanza

Yanga 0 – 0 Biashara United

Dakika ya kwanza Biashara United wanapata penati baada ya Dante Kumuweka chini mchezaji wa Biashara United

Dante anapewa kadi ya njano

Goaaaaaaaal Waziri Junior anaipatia Biashara United bao la Kuongoza

Yanga 0 – 1 Biashara United

Dakika ya 7 Yanga nao wanapata penati baada ya Ibrahim Ajibu kuweka chini ndani ya 18

Goaaaaaaal Dakika ya 8 Amis Tambwe anafunga penati na kuisawazishia Yanga

Yanga 1 – 1 Biashara United

Dakika 15

Yanga 1 – 1 Biashara United

Dakika ya 21 Biashara United wanakosa goli la wazi

Dakika ya 24 Gadiel Michael anajaribu kupiga Shuti langoni mwa Biashara lakini shuti lake linaishia mikononi mwa Kipa

Dakika ya 31 Yanga wanapata kona

Dakika ya 32 Yanga wanapata kona Nyingine

Goaaaaaaaal dakika ya 40 Innocent Edwin anaitanguliza Biashara United kwa bao safi

Yanga 1 – 2 Biashara United

HALF TIME

Yanga 1 – 2 Biashara United

KIPINDI CHA PILI

Kipindi cha Pili kimeanza

Yanga 1 – 2 Biashara United

Dakika ya 46 Mrisho Ngassaa anapewa kadi ya njano baada ya kumchezea madhambi Derrick Mussa

Dakika ya 49 Yanga wanapata Kona wanashindwa kuitumia vyema

Dakika ya 50 Mrisho Ngassa anawekewa pasi nzuri an Ajibu lakini anapiga shuti linalopaa juu ya lango

Dakika ya 59 Mwamuzi Martin Sanya anampa kadi ya Njano Paul Godfrey

Dakika ya 60 Thaban Kamusoko anaingia kuchukua nafasi ya Pius Buswita

Dakika ya 60 Mangalo anapewa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Ngassa

Dakika ya 61 Yanga wanakosa nafasi ya wazi mpira ukabaki kuwa unazengea langoni mwa Biashara kabla ya kipa Nurdin Barola kuudaka

Dakika ya 64 Yanga wanakosa tena bao hapa kichwa cha Makambo kinaokolewa na beki kwenye chaki

Yanga wanapata kona mbili mfululizo

Wanapata Kona nyingine dakika ya 69 lakini kabla ya kuwafikia wachezaji wa Yanga wanamchezea faulo kipa Nurdin Barola

Goaaaaaal Heritier Makambo anaisawazishia Yanga, Dakika ya 73

Ngassa aliingia kwa kasi langoni mwa Biashara United na Kisha akapiga pasi kwa Gadiel aliyemimina Krosi iliyomaliziwa vyema na Makambo

Yanga 2 – 2 Biashara United

Wakati huo huohuo Tambwe ametoka na Matheo Anthony anaingia kuchukua nafasi yake.

Biashara United wanafanya mabadiliko ya kumtoa Kipa Barola anaingia kipa Mwingine Hassan Robert

Baada ya kipa kutolewa anaonekana kumlaumu kocha wake kwanini amemtoaZimeongezwa Dakika 5 kumaliza mechi

FULL TIME

Yanga 2 – 2 Biashara United

PENATI ZINAFATA

Yanga 5 – 4 Biashara United

Yanga wanafuzu hatua inayofuataInstall App bora ya Michezo Tanzania

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY