Mchezaji,Kipa na Mfungaji Bora Sportpesa 2019

Mchezaji,Kipa na Mfungaji Bora Sportpesa 2019

0

Mashindano ya Sportpesa Super cup 2019 yamekamilika leo kwa timu za Kenya kukutana Fainali ambapo ilichezwa fainali kati ya Kariobangi SHARKS ya jijini Nairobi na Bandari Fc kutoka Mombasa

Katika mchezo wa Fainali msomaji wa Kwataunit.co.ke mechi imemalizika kwa Kariobangi Sharks kutwaa ubingwa kwa kuilaza Bandari bao moja kwa sifuri. Huku Simba ikiibuka mshindi wa tatu kwa kuifunga Mbao Fc kwa Penati

Katika michuano hiyo mchezaji bora amekuwa William Wadri kutoka Bandari Fc akiwa mchezaji bora katika mechi mbili kati ya tatu walizocheza Bandari, akiwa mchezaji bora wa mechi kati yao na Singida United na Simba na kutwaa jumla ya dola 1000 sawa na shilingi milioni 2 na laki tatu za Kitanzania.

Mfungaji bora wa michuano hiyo amekuwa mchezaji Duke Abuya wa Kariobangi SHarks huku Kipa bora akiibuka kuwa Metacha Mnata wa Mbao Fc akiwa ameruhusu goli moja tu ndani ya dakika 90 za Mchezo akifungwa na Gor Mahia pekee.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY