Mnamibia Simba aondoka Aussems afunguka hata juu ya uwezo wake na maamuzi

Mnamibia Simba aondoka Aussems afunguka hata juu ya uwezo wake na maamuzi

0

WAKATI Simba ikijiandaa kushuka uwanjani kesho Jumamosi dhidi ya Al Ahly mjini Alexandria, nchini Misri habari kubwa ni juu ya straika Mnamibia Sadney Urikhob aliyetua wiki iliyopita na kufanya majaribio Msimbazi ameonekana kumshawishi Kocha Patrick Aussems.

Mnamibia huyo aliyecheza mechi ya nusu fainali ya SportPesa Super Cup dhidi ya Bandari ya Kenya na Msimbazi kutolewa kwa mabao 2-1, amemkuna Mbelgiji aliyekiri amevutiwa na uwezo wake na anamweka kiporo kwa sasa anamlizane kwanza na Waarabu.

Urikhob alicheza pia mechi ya pili ya kumsaka mshindi wa tatu dhidi ya Mbao FC, huku akionyesha soka tamu na taarifa zilizopo ni kwamba Mnamibia huyo keshasepa kwao, lakini Aussems amesisitiza Urikhob ni mshambuliaji mzuri anayetakiwa kupata muda wa kutosha kufanya mazoezi na wenzake huku akiwa anamuangalia zaidi ya kipindi hiki.

“Mshambuliaji mzuri kwa muda wa siku tatu aliokuwepo kwa mashindano ya SportPesa na amecheza  vizuri na ana uwezo ingawa bado alikuwa mgeni katika timu na hakupata muda wa kutosha kufanya mazoezi na wenzake,” alisema.

“Binafsi ameonesha uwezo mzuri na kwangu nimeona, hivyo ingawa hakuwa na muda wa kutosha kulinana na ratiba yetu ilivyokuwa,” alisema.

“Lakini hata wachezaji wengine hawa watatu ni wazuri ili sikupata muda wa kusha kuwaangalia kutokana akili yangu ipo katika mechi ya Al Ahly, lakini kama kuna ambaye nitakuwa nataka kumuongeza kulingana na mahitaji yangu nitawambia viongozi wamsajili.

“Nimefuatilia wasifu wa kila mchezaji kati ya wote ambao wamekuja kufanya majaribio hapa Simba na hakuna hata mmoja ambaye nimetoa maoni dhidi yake,” alisema Aussems.

Install App bora ya Michezo Tanzania

Mwanaspoti

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY