Muda sahihi wa mechi za Nusu Fainali Sportpesa Super Cup

Muda sahihi wa mechi za Nusu Fainali Sportpesa Super Cup

0

Muda sahihi wa mechi za Nusu Fainali Sportpesa Super Cup

Baada ya Mechi za Juzi jana ilikuwa siku ya mapumziko kwenye michuano ya Sportpesa Super Cup 2019 ila leo shughuli itaendelea katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam kwa mechi za Nusu Fainali.

Mechi zitakuwa mbili leo ambapo mechi ya Kwanza itakuwa kati ya Simba ya Tanzania dhidi ya Bandari kutoka Kenya mechi ikianza saa nane kamili mchana.

Mechi ya Pili msomaji wa Kwataunit.co.ke itakuwa kati ya Mbao Fc “Wabishi” Kutoka Mwanza ambao wataikaribisha Timu ya Katriobangi Sharks kutoka Nairobi Kenya mechi ikianza saa kumi na robo alasiri.

Mshindi wa Kwanza wa michuano hii ataibuka na kitita cha dola elfu thelathini za Kimarekani karibu milioni 70 za Kitanzania.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY