Ole Gunnar Solskjaer aiga Sir Matt Busby

Ole Gunnar Solskjaer aiga Sir Matt Busby

0

Ole Gunnar Solskjaer aiga Sir Matt Busby

Mshambuliaji Mbelgiji Romelu Lukaku aliingia kama nguvu mpya na kufunga mara yake ya kwanza kuugusa mpira na kuwawezesha Manchester United kuwalaza Newcastle United 2-0.

Ushindi wao umemfanya meneja wao mpya Ole Gunnar Solskjaer kuwa meneja wa pili katika historia ya klabu hiyo kushinda mechi zake za kwanza nne.

Raia huyo wa Norway ameiga meneja maarufu Sir Matt Busby aliyefanya hivyo mwaka 1946.

Lukaku, aliyekuwa amekaa uwanjani sekunde 38 pekee, aliupata mpira kufuatia kosa la kipa Martin Dubravka kutoka Slovakia aliyeutema mpira baada ya frikiki iliyopigwa na Marcus Rashford dakika ya 64.

Rashford aliongeza bao la pili dakika ya 80 baada ya uchezaji wa kuridhisha ulioshirikisha Lukaku na Alexis Sanchez ambaye pia alikuwa ameanza mechi akiwa benchi.

Matokeo ya mechi za EPL Jumatano 2 Januari, 2019

  • Bournemouth 3-3 Watford
  • Chelsea 0-0 Southampton
  • Huddersfield 1-2 Burnley
  • West Ham 2-2 Brighton
  • Wolves0-2 Crystal Palace
  • Newcastle 0-2 Man Utd

Newcastle walishindwa kwenye mechi yao ya nane ligini msimu huu.

Nafasi bora zaidi kwa Newcastle ilimwangukia Mhispania Ayoze Perez aliyefanikiwa kuwakwepa walinzi wa Man Utd lakini Luke Shaw akafanikiwa kumzuia.

Wenyeji walikuwa na bahati kumaliza na wachezaji 11 uwanjani baada ya nguvu mpya Jonjo Shelvey kumkaba Paul Pogba kutoka nyuma, lakini hakuadhibiwa na mwamuzi.

Man Utd waendelea kuimarika chini ya Solskjaer

Baada ya ushindi wa kuridhisha dhidi ya Cardiff, Huddersfield na Bournemouth, mechi hiyo ya Jumatano ilikuwa mtihani mkubwa zaidi kwa Manchester United chini ya Solskjaer.

Mechi kama hiyo msimu uliopita, walikuwa wameshindwa 1-0, lakini walicheza vyema sana kwa kushambulia na kuonyesha mchezo wa kupendeza.

Ingawa hakufunga, baada ya kufunga mabao manne katika mechi zake mbili za awali, Pogba alitekeleza mchango muhimu mechi hiyo dhidi ya Newcastle.

Ole Gunnar Solskjaer alisemaje?

“Utafurahi sana ukipata ushindi wa mechi nne kutoka kwa mechi nne – hatujafungwa pia kutoka kwa mchezo wazi.

“Tulianza kwa mwendo pole kiasi kipindi cha kwanza lakini tuliidhibiti mechi vyema, tulikuwa makini sana na kwa jumla ulikuwa uchezaji mzuri.

“Kwa kipindi cha dakika tano, tuliwapa fursa mbili au tatu hivi lakini tukatulia tena.

“Marcus Rashford kidogo anafanana na Cristiano kwa makombora yake, hujipinda na kuyumba, lakini nililipenda bao lake la leo. Alijituliza, na kulitumbukiza wavuni. Hongera.

“Ana miaka 21 pekee, ni lazima ukumbuke hilo. Inakubidi kumchokoza Paul Pogba wakati mwingine na kumzindua, ametufaa sana.”

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY