Simba haipoi huko Congo Balozi awaahidi Mashabiki

Simba haipoi huko Congo Balozi awaahidi Mashabiki

0

Simba haipoi huko Congo Balozi awaahidi Mashabiki

Kikosi cha Simba jana kiliwasili salama mjini Kinshasa Congo tayari kwa pambano lao dhidi ya as Vita Club watoto wa mjini Kinshasa,

Baada ya kuwasili kikosi cha Simba kilipokelewa na balozi wa Tanzania nchini Congo DR Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignac  Mella.

Marcel Kaheza aanza vyema AFC Leopards

Baada ya Kupokelewa Balozi alitia neno na kuwaambia wasishangae wakaona kunawashabiki ambao hawajaenda nao Congo wakiwashangilia.

“Napenda kutumia fursa hii kuwapongeza kwa vile mmejiandaa vizuri nimeona mechi yenu ya kwanza mlipocheza na timu ya Algeria (JS Saoura) mlicheza vizuri sana na kuiweka nchi yetu kwenye ramani nzuri sana”

“Kutokana na uchezaji wenu mahiri, tutaendelea kuwa na nyie na kuwaunga mkono, msiwe na wasiwasi hali ya hapa ni salama kama mlivyoona hakuna vita na hatutegenei vita.”

“Congo nao wanajua Kiswahili kama sisi kwa hiyi wapo pia watawashangilia kwa hiyo msishangae mkiona washangiliaji wamekuwa wengi.”

Baadaye kikosi cha Simba kilifanya mazoezi majira ya Jioni kujiweka Fiti kwaajili ya mchezo huo.

Pata Maujanja ya wakubwa Tu hapa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY