Tetesi za usajili Brani Ulaya leo 28 January 2019

Tetesi za usajili Brani Ulaya leo 28 January 2019

0

Tetesi za usajili Brani Ulaya leo 28 January 2019

Olivier Giroud,32, amesema anaweza kurudi kwenye ligi ya Ufaransa baada ya klabu yake ya sasa Chelsea kumsajili kwa mkopo mshambuliaji Gonzalo Higuain. (Goal)

Winga wa Everton Yannick Bolaise, 29, ameiambia klabu yake kuwa anataka kutoka tena kwa mkopo baada ya kukatisha mkataba wake wa mkopo na Aston Villa. Klabu za Newcastle, Burnley na Cardiff zinammezea mate mhezaji huyo. (Mirror)

Paris St-Germain wametangaza dau la pauni milioni 21.5 kumsajili kiungo wa Everton Idrissa Gueye – lakini Everton imekataa ofa hiyo na kusema mchezaji huyo mwenye miaka 29. (Sky)

Kiungo wa Leicester Adrien Silva, 29, anataka kuondoka klabuni hapo kabla ya dirisha la usajili mwezi huu kufungwa. Silva hajawahi kupangwa kwenye kikosi cha kwanza katika Ligi ya Premia tika msimu huu ulipoanza. (Guardian)

Kocha mpya wa klabu ya Stoke Nathan Jones anataka kukipa nguvu mpya kikosi chake kwa kukaribisha ofa za timu zinazowataka wachezaji wake wakongwe watatu – Bojan, Darren Fletcher na Peter Crouch – ambao ndio wanaopokea malipo makubwa Zaidi klabuni hapo. (Daily Mail)

Beki wa West Ham Reece Oxford, 20, anatakiwa na kocha Martin O’Neil wa klabu ya ligi ya daraja la kwanzaya Nottingham Forest, klabu hiyo imetenga kitita cha pauni milioni 8 ili kumnasa kinda huyo. (Mirror)

Oxford tayari ameshacheza kwa mkopo katika ligi ya Ujerumani, Bundesliga, na klabu ya Eintracht Frankfurt pia wameonesha nia ya kumsajili karika dirisha la usajili la mwezi huu. (Sky)

Ben Woodburn, 19, ambaye ni mchezaji anayeshikilia rekodi ya kufunga bao akiwa na umri mdogo zaidi katika historia ya Liverpool anaweza kujiunga na klabu ya Hull kwa mkopo baada ya kumaliza muda wake wa mkopo na Sheffield United. (Daily Mail)

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY