Tetesi za Usajili Ulaya leo 17 January 2019

Tetesi za Usajili Ulaya leo 17 January 2019

0

Tetesi za Usajili Ulaya leo 17 January 2019

Chelsea wameamua kumsajili Gonzalo Higuain baada ya Juventus kukubali ofa yao. Mshambuliaji huyo raia wa Argentina alikuwa akichezea AC Milan kwa mkopo. (Telegraph)

Atletico Madrid wanakaribia kumsaini mshambuliaji wa Chelsea lvaro Morata, 26, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa euro milioni45. (Sky Sports)

Arsenal wako tayari kutumia sehemu ya mshahara wa Mesut Ozil endapo watafanikiwa kumuuza ili kumsajili mchezaji mwingine.

Ozil ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika klabu hiyo. (Mirror)

West Ham wanapania kumnunua mshambuliaji wa Celta Vigo na Uruguay Maxi Gomez, 22, kujaza pengo litakaloachwa na Marko Arnautovic. (Sky Sports)

Manchester City huenda wakapoteza nafasi ya kumsajili Frenkie De Jong kutoka Ajax baada ya Paris St-Germain kuonyesha azma ya kutaka kumununua kiungo huyo.

Japo De Jong wa miaka 21 angelipendelea ujiunga city chini ya Pep Guardiola, PSG ndio klabu pekee ambayo iko tayari kulipa Ajax euro milioni 66. (Mirror)

Chelsea wanataka kumuuza mshambuliaji wao Michy Batshuayi, 25, kwa Everton kwa kima cha euro milioni 40.

Everton wanaweza tu kumsajili mshambuliaji huyo wa Ubelgiji kwa mkataba wa kudumu kwasababu tayari wamemsajili mlinzi wa Ufaransa Kurt Zouma, 24, kwa mkopo kutoka Chelsea. (Star)

Batshuayi anataka sana kukamilisha mkopo wake ili aweza kuhamia Monaco. (Telegraph)

Kipa wa Uhispania David de Gea, 28, anatarajiwa kutia saini mkataba mpya na Manchester United. (Mirror)

Wachezaji wa Chelsea Alvaro Morata, 26, na Olivier Giroud, 32, Fernando Llorente, 33,wa ,Tottenham na Lucas Perez, 30, and Girona’s Cristhian Stuani, 32, wa West Ham wako katika orodha ya Barcelona ya wachezaji wa ziada wanaotarajiwa kusajiliwa na klabu hiyo. (Mail)

Manchester United huenda wakamsajili winga wa PSV Eindhoven Steven Bergwijn huku wakiwa na lengo la kuweka dau la euro milioni 25 kumnunua kiungo huyo raia wa Ujerumani mwezi huu. (Sun)

Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Ubelgiji Divock Origi, 23, ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Tottenham baada ya Harry Kane, 25, kuumia. (Telegraph)

Tottenham wamepanga mkutano wa ngazi ya juu kujadili jinsi watakavyo kabiliana na ukosefu wa Kane uwanjani kwa miezi kadhaa.

Kuna uwezekano wakawasaini wachezaji wapya au kumpandisha cheo mshambuliaji Troy Parrott mwenye umri wa miaka 16. (Talksport)

Bayern Munich pia wanafanya mazungumzo ya kumsajili winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi. (Bild via Four Four Two)

Kipa wa Liverpool Simon Mignolet, 30, anatazamiwa kusalia katika klabu hiyo hadi mwisho wa msimu huu. (ESPN)

Juhudi ya Hull City ya kumnunua mlinzi wa Cardiff Matthew Connolly, 31, zimegonga mwamba. (Hull Daily Mail)

Cardiff City wanakaribia kufikia mkataba wa wa kumsajili mshambuliaji wa Nantes Emiliano Sala, 28, kwa kima cha karibu uero milioni 18. (Sky Sports)

Chelsea wako tayari kumpatia kazi kipa wao wa zamani Petr Cech ambaye anastaafu mwisho wa msimu huu.

Cech ambaye kwa sasa ni kipa wa Arsenal, alitangaza hatua ya kustaafu kwake Jumanne wiki hii.

Kiungo huyo wa zamani wa Chelsea huenda akapewa kazi ya ukufunzi au ya balozi mwema(Times)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City na Liverpool Mario Balotelli anajiandaa kujiunga na Marseille kutoka Nice.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 28, amekuwa akichezeaNice inayoshiriki Ligue 1 tangu alipohama Liverpool kwa mkopo mwaka 2016.

Mkataba wa Balotelli katika klabu ya Nice unakamilika mwisho wa msimu huu.

Wakubwa Wanafaidi – Install App Ujionee

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY