Walichokisema Yanga leo kwenye mkutano kuhusu Kakolanya

Walichokisema Yanga leo kwenye mkutano kuhusu Kakolanya

0

Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kaimu mwenyekiti wa klabu hiyo Samwel Lukumay umesema kwamba mlinda mlango Beno Kakolanya haidai klabu hiyo katika kipindi hiki baada ya kumaliziwa stahiki zake ambazo amekuwa akizidai.

Lukumay ameongea hii leo Katika mkutano na Waandishi wa Habari, amesema kwamba uongozi siku ya jana umepokea barua kutoka kwa wanasheria wa Beno wakihitaji kuvunja mkataba wake jambo ambalo amedai uongozi utakaa na kulijadili kwa undani kwani mchezaji alishalipwa stahiki zake kabla ya madai hayo ya kuvunja mkataba.

Install App bora ya Michezo Tanzania

Amesema kwamba kimsingi hadi kufikia sasa mchezaji ni wa Yanga hivyo kama dhamira yake ni kuvunja mkataba basi ni vizur taratibu zikafuatwa.

Aidha amesema kwamba swala la yeye na kocha mkuu wa klabu Mwinyi Zahera ni jambo ambalo mchezaji alipaswa kuwasiliana na uongozi au kocha mwenyewe ili kulipatia ufumbuzi jambo ambalo hakulifanya.

Kwa mujibu wa Lukumay amesema kwamba katika usajili wa msimu uliopita Beno amesaini mkataba wa miaka miwili hivyo bado angali na mkataba wa muda mrefu kusalia ndani ya klabu hiyo.

“Kakolanya alishindwa kujiunga na timu wakati tunakwenda kucheza na Mwadui na mwenzake Kelvin Yondani ila Yondani alirejea yeye akashindwa kurejea zaidi ya kutuandikia barua ya kuomba alipwe stahiki zake na kusitisha mkataba na timu.

“Baada ya mazungumzo tulikubaliana tumlipe stahiki zake ili arejee ndani ya timu ila hakuweza kufanya hivyo baada ya kuanza kulipwa stahiki zake bila kutoa taarifa yoyote, hali iliyopelekea kocha mkuu Mwinyi Zahera kumkataa.

“Tarehe 25 alituandikia barua nyingine kupitia kwa mwanasheria wake akihitaji kuvunja mkataba wake na ilikuwa ni barua ya msisitizo ambayo tuliipokea tarehe 28 hivyo kwa sasa bado tunaendelea kuitendela kazi kwa kuwa ni masuala ya kisheria,”

Install App bora ya Michezo Tanzania

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY