Zahera afunguka kuhusu uwezo wa Gustafa Simon

Zahera afunguka kuhusu uwezo wa Gustafa Simon

0

Zahera afunguka kuhusu uwezo wa Gustafa Simon

UWEZO unaoonyeshwa na kiungo kinda wa Yanga B, Mustafa Simon ‘Kante’, kwe-nye michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, umemkuna vilivyo kocha mkuu wa kikosi hicho, Mwinyi Zahera.

Kinda huyo alianza kuonyesha cheche zake mchezo wa kwanza tu katikati ya wiki dhidi ya KVZ Wanajangwani wali-poibuka na ushindi wa bao 1-0.

Ratiba ligi kuu TPL leo 6 January 2019

Zahera alituambia , anafurarahia uwezo wa wachezaji wake hao waliopo visiwani humo, huku kundi kubwa wakiwa ni makinda kutoka timu B, huku akimmwagia sifa zaidi Kante.

“Walionyesha kiwango kizuri mchezo wa kwanza, Saimon (Mustafa) ana kipaji kikubwa, ukifika muda wake atapanda timu ya wakubwa, ingawa nafasi anayo-cheza wapo wengi,” alisema.Kinda huyo huenda akafuata nyao za wenzake, Maka Edward na Paul Godfrey ambao wapo kikosi cha wakubwa hivi sasa ambapo wamekuwa wanapta nafasi mara kadhaa ya kushuka dimbani.

Credit : Dimba

Like ukurasa wetu wa Facebook Hapa kwa habari zaidi

Install Simba na Yanga Breaking News App

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY