Zahera asema hata wapige kelele hili hafanyi Yanga

Zahera asema hata wapige kelele hili hafanyi Yanga

0

Zahera asema hata wapige kelele hili hafanyi Yanga

Kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera siku kadhaa zilizopita alitangaza maamuzi mapya ya kumtengua Kelvin Yondani na majukumu yake kumpa Ibrahim Ajibu kama nahodha Mpya wa Yanga.

Zahera alisema alimuonya Mara nyingi Yondani kuhusu kubadilika kuhusu nidhamu yake lakini Yondani hakubadilika na kuamua kufanya maamuzi hayo.

Erasto Nyoni amchanganya Aussems Afunguka haya

Zahera alisema baada ya kumchagua Ajibu watu wengi wamekuwa wakiongea mengi wakitaka abadilishe maamuzi lakini yeye kama kocha hatasikiliza kelele zao na hawezi kubadili maamuzi aliyofanya.

Zahera amewataka watu wa Yanga kumsapoti Ajibu na mwenzake Juma Abdul huku akiweka wazi kuwa moja ya sababu za kumpa unahodha Ajibu ni mabadiliko ya Ibrahim Ajibu ambayo amekuwa akiyafanya ambayo wengi waliamini Ajibu hawezi kubadilika lakini amebadilka.

Like ukurasa wetu wa Facebook Hapa kwa habari zaidi

Install Simba na Yanga Breaking News App

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY