Zahera ataja wachezaji asiowataka Yanga

Zahera ataja wachezaji asiowataka Yanga

0

Zahera ataja wachezaji asiowataka Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameweka wazi aina ya wachezaji ambao yeye angependa kufanya nao kazi katika kikosi cha Yanga na vile vile amewataja wale asiowahitaji.

Zahera ambaye juzi alimvua unahodha Kelvin Yondani na kumkabidhi Ibrahim Ajib, amesema kitu cha kwanza  anachokihusudu ni nidhamu kwa kila mchezaji.

Amesema yeye haangalii jina la mtu na badala yake yule anayetii na kuendana na matakwa ya timu, ndio watakaokwenda sawa, lakini ikitokea vinginevyo hakawii kutoa uamuzi mgumu.

Zahera asema hata wapige kelele hili hafanyi Yanga

“Kila mchezaji anatakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu, hiyo ni moja ya sababu inayoweza kuifanya timu kufikia malengo, lakini kila mmoja akijiamulia mambo hayawezi kwenda vizuri,” alisema.

Pia alisema aina nyingine ya mchezaji anayeweza kuishi na kufanya naye kazi vizuri ni yule anayejituma mazoezini na kuzingatia kile anachofundishwa.

Alisema mbali na hilo, pia anawapenda wachezaji wenye uvumilivu tofauti na wale ambao wakipata shida kidogo wanakata tamaa na kuacha mazoezi.

Zahera amekuwa na misimamo mikali hasa kwa wachezaji ambao hawaendi naye sawa, akiwamo kipa Beno Kakolanya, aliyepigwa marufuku kujiunga na timu kwa madai ya kukacha kwenda mazoezini huku Yondani akivuliwa unahodha akidaiwa kuchelewa kurudi kutoka kwenye mapumziko.

Yanga ndio wanaoongoza Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 40 wakicheza michezo 18 wakishinda michezo 16, sare michezo miwili ikiwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote

Like ukurasa wetu wa Facebook Hapa kwa habari zaidi

Install Simba na Yanga Breaking News App

source : Dimba

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY