Zahera atangaza mechi za Ubingwa

Zahera atangaza mechi za Ubingwa

0

Zahera atangaza mechi za Ubingwa

BAADA ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mwadui FC, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameweka wazi kwamba ana mechi nne za kumtengenezea njia ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Akizungumza baada ya mchezo huo wa Ligi Kuu uliochezwa juzi Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Zahera, alisema amefurahi kushinda mechi hiyo.

Zahera alisema kutokana na mazoezi magumu waliyofanya wiki mbili zilizopita, alijua kama mechi yao hiyo ingekuwa ngumu sana ila ushindi huo umewapa picha ya kile walichofanya.

“Nafurahi tumeshinda, kutokana na mazoezi ya nguvu tuliyofanya kwa wiki mbili tukajua mechi hii itatusumbua sana, lakini tumeshinda imetusaidia,” alisema kocha huyo.

Zahera aliongeza kuwa kutokana na mazoezi hayo wakishinda mechi nyingine nne wapinzani wake itakuwa ngumu sana kumkuta.

“Kama tukiendelea kucheza mechi nne kama hivi na kushinda, itakuwa ngumu sana kutufikia,” alisema kocha huyo wa DR Congo.

Zahera ametamba kuwa amewafanyisha wachezaji wake mazoezi mazito ya mechi 10 katika kipindi hicho cha wiki mbili.

Kwasasa Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 53, baada ya kucheza mechi 19 na kushinda 17 na kutoka sare mbili.

Wakubwa Wanafaidi – Install App Ujionee

Bingwa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY