Zahera ateka kampeni za Uchaguzi Yanga

Zahera ateka kampeni za Uchaguzi Yanga

0

Kibarua cha Kocha Mkongo, Mwinyi Zahera kimegeuka gumzo kwenye kampeni za mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti Yanga Dk Jonas Tiboroha.


Mgombea huyo aliulizwa endapo atapewa ridhaa ya kuongoza Yanga, nafasi ya Zahera katika kufanya uamuzi kwenye kikosi cha Yanga itaendelea kama ilivyo sasa au uongozi utamvuruga na uongozi kubeba jukumu lake ikiwemo kumwingilia katika maamuzi yake.


Akijibu swali hilo, Tiboroha alisema kwenye ‘ishu’ ya Zahera ni kocha ambaye ameiweka Yanga kwenye misingi imara.


“Kwa Zahera lazima niwe mkweli, tutakuwa watu wa ajabu tukiingia pale tukamwondoa kwenye timu, kwani ujio wake kwanza umeisogeza timu kwa wanachama. Lakini pia Zahera atoingiliwa majukumu yake atapanga mwenyewe na sisi tutashauri tu,”alisema Tiboroha.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY