Zahera awaambia Simba wasahau hili

Zahera awaambia Simba wasahau hili

0

Zahera awaambia Simba wasahau hili

Kocha Mkuu wa timu ya Yanga ambaye amekuwa maarufu nchini kutokana na matokeo ambayo amekuwa akiipatia Yanga na misimamo ambayo amekuwa akiwanyao juu ya kikosi cha Yanga.

Kocha huyo alifunguka kuwa kwasasa Simba wasahau kucheza kwa kujilinda muda wote kama walivyocheza katika mechi ya mzunguko wa Kwanza wa Ligi walipokutana.

Zahera alisema anajivunia kikosi chake cha sasa kutokana na ongezeko la wachezaji kama Boban na Mo Banka ambao hawakuwepo katika mchezo wa Kwanza lakini pia anajivunia kuendelea kuimarika kwa kikosi chake.

“Wakati wa mzunguko wa kwanza nilikuwa naogopa kucheza na Simba ndiyo maana tulipokutana nao tulijilinda sana, kwa sababu wao walikuwa na kikosi kikubwa zaidi kuliko kile cha kwetu na walikuwa na wachezaji wazuri.

“Lakini kwa sasa sina hofu tena ya kucheza nao hata kidogo kwa sababu tumeboresha timu na tumefanya usajili wa Boban ambaye amekuja kutusaidia na kuongeza nguvu.

“Lakini pia kwa sasa tuna kikosi kikubwa na jambo zuri kabla ya kukutana nao, pia Banka naye atakuwa tayari yupo kwenye timu yetu, utaona ni kikosi gani ambacho nitakuwa nacho wakati ambao tutacheza na Simba katika mzunguko wa pili,” 

Like ukurasa wetu wa Facebook Hapa kwa habari zaidi

Install Simba na Yanga Breaking News App

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY