Alichokisema Zahera baada ya kupoteza mchezo na Simba

Alichokisema Zahera baada ya kupoteza mchezo na Simba

0

Alichokisema Zahera baada ya kupoteza mchezo na Simba

Jana klabu ya Simba iliweza kumaliza kelele za Yanga kwa kuwafunga bao 1 kwa 0 na kuongeza points 3 muhimu na kuzidi kuongeza matumaini ya kuweza kutetea Ubingwa wake.

Baada ya mchezo huo msomaji wa Kwata unit kocha wa Yanga Zahera Mwinyi alifunguka kuwa ameshindwa kuwafunga Simba kwasababu walikuwa bora kuliko wao lakini akiamini bado wananafasi ya kufanya vizuri michezo iajyo.

“Nimeshindwa kuwafunga Simba kwa kuwa walikuwa bora na wachezaji wake wana akili uwanjani, ila mimi sishangai na wala siwalaumu wachezaji wangu wamecheza kwa juhudi licha ya kufungwa leo.

“Nimewaona Simba wakiwa uwanjani walikuwa wanatafuta bao licha ya kuwadhibiti, bado tuna nafasi ya kufanya vizuri michezo yetu ijayo endapo nitapata wachezaji bora ambao ninawahitaji ” alisema Zahera

Install App bora ya Michezo – Michezo Plus App

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY