Habari mpya kutoka Yanga leo 22 February 2019

Habari mpya kutoka Yanga leo 22 February 2019

0

Habari mpya kutoka Yanga leo 22 February 2019

Kikosi cha Wachezaji 20 Yanga leo kitasafiri kuelekea Ruangwa mkoani Lindi kuifuata Nmungo Fc ya Mkoani Lindi katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa tarehe 24 February 2019.

Mchezo huo ni wa kombe la Azam Sports Federation Cup, Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amefunguka kuwa kikosi kitaondoka leo kwa basi kuelekea Lindi.

“Maandalizi ya timu yetu yanaendelea vizuri na kikosi kipo fiti kwa ajili ya mchezo wetu huo wa FA, tunafahamu ratiba inatubana, lakini tutajitahidi kuhakikisha tunapata ushindi.


“Timu imerejea jana asubuhi kutoka Mwanza kwa ndege tukitoka kuvunja mwiko kwa kuifunga Mbao nyumbani, hivyo nguvu na akili zetu tunazielekeza mchezo dhidi ya Namungo.


“Tunatarajia kusafiri kesho leo alfajiri kwa basi letu tunalolitumia kuelekea huko Ruangwa tayari kuwakabili wapinzani wetu Namungo, tuna kibarua kigumu katika mchezo huo lakini hatuna hofu tutapata ushindi kutokana na ubora wa timu yetu,”alisema Saleh.

Install App Bora Ya Michezo Hapa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY