Hadithi : Mama Vanessa – Sehemu ya Kwanza

Hadithi : Mama Vanessa – Sehemu ya Kwanza

0

SEHEMU YA KWANZA

Muda ulikuwa umeenda sana macho ya Lucas Manyama yalianza kujifumba yenyewe ishara kuwa mwili wake ulikuwa umechoka na ulihitaji kupumzika. Saa yake ya ukutani ilionenesha kuwa ilikuwa ni saa 8 usiku na alikuwa anasoma story pendwa inayoitwaSECRET OF LOVE iliyotungwa na mtunzi maarufu kwa jina Eliado. Nia ya kusoma story hii usiku ni kupunguza mlundikano wa mawazo aliyokuwa nayo na kutafuta faraja kupitia matatizo ya wengine..Siku hiyo pia ni siku ambayo alikuwa na sress nyingi sana ambazo kwa yeye alihisi kuwa zilikuwa zinamzidi umri. Kwanza ni siku ya 6 tangu asimamishwe kazi kutokana na tuhuma za uwongo ambazo boss wake alijaribu kumbambikizia. Si kusimamishwa kazi tu bali pia mke wake kuondoka nyumbani kwa madai kuwa amemchoka. Ilikuwa haimuingii akilini kuwa eti mke wake amechoka na kuamua kumuacha katika kipindi hiki kigumu.

“Kwa nini hakunichoka kipindi nikiwa nina kazi? kwa nini hakuondoka kipindi hicho? nini kimemfanya aondoke?”Aliwaza Lucas bila kupata majibu. Usingizi kwake ulikuwa ni mgumu sana na alitamani hata asilale. Mziki wa taratibu ulitosha kabisa kuelezea ni jinsi gani alivyokuwa anakijisikia. Machozi yalitosha kabisa kulowanisha karatasi za kitabu cha story alichokuwa anasoma. Badala ya kufuatilia kitabu hicho ambacho kilikuwa ni kizuri alikuwa amekishika kama pambo na wala alikuwa haelewi kilichoandikwa. Alikuwa na huzuni iliyopitiliza. Alitamani hata kama asubuhi ingefika alione jua alihisi labda kuliona jua kungefanya roho yake kutulia. Alijawa na hisia kuwa giza la usiku huo lingeweza kumuathiri kwa kiwango kikubwa. Mvinyo wa kizungu aliokuwa anakunywa hakuweza hata kuusikia, alikunywa kama maji.

Alikunywa hakulewa.Kila alipokuwa anavuta kumbukumbu ya yaliyomtokea alilia kilio kisicho na machozi.

“Nilimpa kila kitu nilimpenda kupita vitu vyote lakini leo ananiacha?” aliwaza bila kupata majibu.

Huyu mwanamke alikuwa ni kila kitu kwake, huyo mwanamke alimtoa mbali, huyo mwanamke alikuwa na umuhimu sana maana kwake alikuwa kama mama na hii ni baada ya kumpoteza mama yake mzazi ambaye aliitwa na Mungu.Apumzike kwa amani mama yake mpendwa.

“Huyu mwanamke nilimsomesha kwa gharama zangu huyu mwanamke nilimwinua kutoka familia masikini mpaka akafikia hapo alipo. Hiyo kazi anayoringia ni sawa tu mimi ndio niliyomuwezesha kwa maana bila elimu niliyomsadia kuipata hasingekuwa hapo.Lakini kwa nini sasa hataki kuyatambua hayo. Kwa nini athamini mchango wake kwangu?”.

Manyama aliongea kwa nguvu utafikiri labda huyo mwanamke wake alikuwa hapo. Alinyanyua glass ya kinywaji kikali alichokuwa akinywa na kukidigida utadhani sio kilevi. Mara simu yake iliita na aliangalia kwa haraka maana sio kawaida yake kupigiwa simu usiku. Aliichukua simu ambayo ilikuwa kwenye chaji na kuipokea.

“Helow mambo Lucas” ilisiskika sauti nyororro sauti ya kike iliyojaa bashasha na furaha.

“Mambo poa, sijui naongea na nani?”.

“Jamani mbona unaharaka hivyo, mimi najua hunijui lakini utanijua maana ni zaidi ya malaika niliyetumwa na Mungu nije kukukomboa na kukuondoa kwenye upweke uliokuwa nao”.

“Makubwa kumbe kuna binadamu malaika..Utanisamehe kama huwezi kujitambulisha sitoweza kuongea na wewe.” Lucas alijibu kwa hasira na kukata simu.

Kama hiyo haitoshi aliamua kuizima kabisa, alivurugwa akavurugika.Alihisi kabisa walikuwa ni vibaraka wa mkewe Misheli walitumwa kumkejeli.Pamoja kuwa alichukua maamuzi hayo bado roho ilimsuta kwa jinsi sauti hiyo ya kike ilivyokuwa tamu masikioni mwake. Alitamani sana kumjua mwanamke huyo lakini hakutaka kuwasha simu. Alijitupa kitandani na kuanza kuutafuta usingizi ambao takribani wiki nzima alikuwa akiupata kwa shida sana. Aliendelea kuwaza vitu vingi sana ikiwa ni pamoja atapata wapi pesa ya kodi kwa sababu mwezi huo ndo ulikuwa wa kulipa kodi hili hali amesimamishwa kazi kwa sababu ambazo ni za kusingiziwa.

“Yaani Boss Yule mwanamke ni mchepuko wake tu je ingekuwa ni mke wake si angenifunga jela kabisa.Mwanamke mwenyewe hamtaki anataka vijana wezniye yeye kazi kuonga tu. Faidha ametamka kwa kinywa chake kuwa hampendi boss bali mimi sasa mimi ningefanyaje. Yaani mwanamke mzuri kama Faidha amejilengesha mwenyewe mimi nimwache kisa eti ni mchepuko wa boss ambaye hajawahi kulala naye?”.Manyama aliendelea kuwaza na kuwazua.

“Akafu mke wangu alijuaje yote haya yanayoendelea kazini?. Na kwa nini hakuniuliza akaamua kuondoka kimya kimya bila hata kuniambia sababu. Nimepiga simu mpaka nyumbani kwao hawapokei tatizo ni nini hasa?”.

Maswali yote hayo hayakuwa na majibu kwa kijana huyu. Alifikiria jinsi kupata kazi ilivyokuwa ngumu. Alifikiria kuwa hata kazi hiyo aliipata kwa msaada wa mjomba wake. Ni kweli elimu yake ilikuwa nzuri kuliko wafanyakazi wengine na hata utendaji wake wa kazi ulikuwa na ufanisi mkumbwa kuliko wengine. Tatizo kumbwa ni mfanyakazi mpya wa mambo ya masoko aliyeletwa hapo kazini kwao. Msichana huyu alikuwa mrembo kupita kiasi. Urembo wa Faidha ndo huo ulileta kizaazaa katika taasisi yao. Lucas Manyama ni mfanyakazi wa benki moja ya kibiashara mkoani Mara. Ni miezi 3 tu tangia apate kazi hiyo na katika muda huu mfupi ndo analetwa Faidha binti ambaye alimvutia kila mwanaume hapo benki. Boss naye alikuwa mtu aliyevutiwa na mfanyakzi huyo na yeye alitumia cheo chake kumshawishi na kutaka kuwa naye. Lakini Faidha alikuwa ni mwanamke mjanja sana bado aliangalia future yake. Ni msichana ambaye hakupenda kujihusisha kimauhusino na wazee.

Lakini moyo wake ulivutiwa na kijana Lucas ambaye alikuwa ni kipenzi cha wafanyaakzi wengi na wateja kutokana na ufanisi wake wa kazi kuwa uliotukuka. Hali hii ilijenga ukaribu sana na kupeleka kujikuta wakizama kwenye uhusiano bila kutajaria. Faidha alijua kabisa kuwa Lucas alikuwa na mke ambaye naye ni mfanyakazi wa taasisi nyingine hapo hapo Musoma. Wote waliingiwa na upofu ambao kwa kweli ulileta majanga makumbwa kwa upande wa Lucas. Lucas alijiuliza kama walifanya siri yeye na Faidha imekuwaje mkwe akajua na kuamua kuondoka. Mkewe aliondoka ghafla bila kutoa sababu yoyote na kipindi hiko tayari alishasimamishwa kwa kazi kwakile kilichoitwa ubadhilifu wa fedaha. Kitu kingine kilichokuwa kikumuuama ni kuwa Boss na mkewe walikuwa wakijuana maana walitoka mkoa mmoja na walikuwa karibu.

Lucas Manyama alihisi labda Boss ameamua kumwaga sumu kwa mkewe na ndio maana ameondoka. Alichokifanya alilala na asubuhi na mapema aliamka na kuelekea ukweni ambapo ni Bukoba. Aliamua kwenda ili kujua kama mke wake alirudi huko au la kuna sehemu ambayo alienda bila yeye kujua. Ila ile simu alivyoiwasha asubuhi hiyo alikutana na meseji nyingi za yule mwanamke aliyempigia simu usiku huku akijichkesha chekesha.

“Lucas najua upo katika kipindi kigumu sana, kipindi cha mawazo lakini mini mimi ndo naweza kukufumbua macho na kujibu maswali yako yote magumu yanayokutatanisha. Hata mimi nina maumivu sana ila naomba tushirikiane nitakufuta machozi na pia nitakufanya ujue ukweli kuhusu mkeo na boss wako..Ukiwa tayari tafadhali nitafute naitwa mama Vanessa.” Meseji ilisomeka hivyo na kumfanya Lucas hazidi kuchangnyikiwa. Alitamani kushuka kwenye gari lakini aliamua kuendelea na safari ya ukweni maana ingetoa mwanga pia kwa nini mkewe aliamua kuondoka tena kimya kimya…

********ITAENDELEA******

Mwendelezo wa Sehemu zinazofuata Ukitaka Zipo Hapa Bonyeza Hapa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY