Julio : Yanga wataifunga Simba

Julio : Yanga wataifunga Simba

0

Julio : Yanga wataifunga Simba

KOCHA wa Dodoma FC ambaye ameshawahi kuichezea na kuifundisha Simba, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’, amefunguka kuwa Yanga wanayo nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa Jumamosi kutokana na watu wengi kuwadharau.

Yanga atakuwa dimbani kucheza dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, ambao unategemewa kuwa na ushindani huku wadau wengi wakiipa nafasi zaidi Simba kuibuka na ushindi hasa kutoka­na na matokeo ya bao 1-0 waliyovuna kwa Al Ahly.

Akizungumza naSI Julio alisema kuwa watu wasi­idharau Yanga kwa sababu ya ushindi wa Simba dhidi ya Waarabu, kwa kuwa historia ya michezo hiyo inaonyesha kwamba timu inayoonekana dhaifu ndiyo inapata ushindi.

“Simba atafungwa hii mechi kwa sababu wachezaji na benchi la ufundi wamezidi kujiamini sana kutokana na kuwa na kikosi kipana, lakini kubwa ushindi waliopata dhidi ya Waarabu.

“Wanasahau kuwa mich­ezo ya Simba na Yanga huwa haitabiriki na mara nyingi timu ambayo inaonekana mbovu ndiyo upata matokeo ya ush­indi,” alisema Julio.

Install App bora ya Michezo – Michezo Plus App

source : Champion

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY