Kagere anogewa awataka na Yanga

Kagere anogewa awataka na Yanga

0

Kagere anogewa awataka na Yanga

Straika wa kutumainiwa wa klabu ya Simba Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda Meddie Kagere amefungyuka kufurahishwa kwake kuwafunga Al Ahly na kuahidi kuendeleza moto hata katika mchezo wa yanga Jumamosi.

Akiongea baada ya mechi hiyo Kagere alisema goli alilowafunga Al Ahly limezidi kumpa hamasa na kuona kuwa anadeni la kuwafunga na Yanga katika mchezo unaofuata wa Ligi kuu.

“Bao nililowafunga Al Ahly linaweza kuwa kichocheo cha kutaka kuendelea kufunga na natamani kufunga katika mchezo unaofuata dhidi ya Yanga ” alisema Kagere

Yanga ndiyo watakaokuwa wenyeji wa mchezo huo utakaofanyika Jumamosi 16 February 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

Install App bora ya Michezo – Michezo Plus App

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY