Kwa dau hili walioahidiwa wachezaji Simba na Mo Waarabu kazi wanayo

Kwa dau hili walioahidiwa wachezaji Simba na Mo Waarabu kazi wanayo

0

Kwa dau hili walioahidiwa wachezaji Simba na Mo Waarabu kazi wanayo

LOLOTE liwe kudaadek! Jumamosi Simba itakuwa uwanjani kuivaa Al Ahly katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini habari nzuri ni kuwa bilionea wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ ni kama tayari amemaliza majukumu yake kwa asilimia kubwa na kilichobaki ni wachezaji wa Simba kumaliza kazi.

Mchezo huo umekuwa gum­zo hasa kutokana na kiwango cha Simba katika siku za hivi karibuni kuonekana kuyumba lakini kuelekea mtanange huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Borg El Arab ndani ya Mji wa Alexandria, maandalizi ya Simba yamekamilika kwa asil­imia kubwa.

Ikiwa Simba itafanikiwa kupata ushindi kesho, utawawezesha kujikusanyia mamilioni ya fedha kutoka kwa Mo ambaye inad­aiwa amewaahidi donge nono, hali ambayo imeongeza morali kwa asilimia kubwa kambini hapo.

Akizungumza nasi Mtendaji Mkuu wa Simba (CEO), Crescentius Magori alisema kuwa endapo wachezaji hao watafanikiwa kupata ush­indi katika mchezo huo wame­andaliwa donge nono la fedha.

“Kuna ahadi kweli ya fedha ambayo tumeahidi wachezaji wetu kuwa tutawapatia endapo watapata ushindi katika mechi hiyo kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote lakini kwa hii itakuwa tofauti kidogo.

“Kwa hiyo ni wajibu wao kupambana uwanjani ili kuhakikisha tunapata ushindi lakini pia kitita hicho cha fedha ambacho wao wanajua kuwa tumewaahidi kuwa­patia mara tu wataka­poshinda,” alisema Magori.

Hata hivyo, habari za kuaminika kutoka kwa mmoja wa wachezaji wa timu hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, zinase­ma kuwa, endapo watashinda mechi hiyo, kila mchezaji aliyecheza ataondoka na kikita cha Sh 4,000,000.

“Kabla ya kuja huku tulifanya kikao na uongozi na ukatu­ambia kuwa tukishinda kila mchezaji aliyecheza atapata Sh 4,000,000 na ambaye alikuwa benchi lakini hakucheza ata­chukua Sh 3,000,000.

“Wale ambao hawakusafiri na timu pia watapewa Sh 1,000,000 kila mmoja, kwa hiyo ni lazima tupam­bane uwanjani kwa nguvu zote ili kuhakiki­sha tunashinda.

“Lakini pia mbali na kupata fedha hizo, ush­indi huo tutakaoupata utatusaidia kurudisha imani kwa mashabiki wetu ambayo hivi karibuni walituchukia kutokana na matokeo mabaya tuliyoyapata baada ya kufun­gwa mabao 5-0 na AS Vita ya DR Congo, lakini kiwango cha chini tulichokionyesha kwenye michuano ya Sport­Pesa,” alisema mchezaji huyo.

Install App bora ya Michezo Tanzania

source : Champion

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY