Matokeo TPL Mbao Vs Yanga leo

Matokeo TPL Mbao Vs Yanga leo

0

Matokeo TPL Mbao Vs Yanga leo

Matokeo ya Moja kwa Moja kati ya Mbao Fc dhidi ya Yanga ligi kuu soka ya Tanzania Bara TPL leo 20 February 2019

Mechi Imeanza

Mbao 0 – 0 Yanga

Dakika ya 1 Mbao wanaanza kwa shambulizi Shuti la Said Said Jr linapaa

Dakika ya 2 Yanga wanafanya Shambulizi zuri lakini Krosi ya Mrisho Ngassa inaishia Mikononi mwa Kipa Metacha Mnata

Dakika ya 3 Mbao Fc wanajaribu shuti langoni mwa Yanga lakini mpira unaenda nje ya lango

Dakika ya 7 Mbao Wanapata Kona baada ya Yondani kumrudishia mpira mrefu uliomshinda Kabwili na Kutoka.

Inapigwa kona kabwili anautoa na kuwa kona Nyingine, Lakini wanashindwa kuitumia

Dakika ya 8 Yanga wanatengeneza nafasi nzuri lakini tayari wanakuwa wameshaotea

Dakika 15

Mbao 0 – 0 Yanga

Mbao Fc wanaonekana kulishika eneo la Kati ya Uwanja kutokana na kujaza Viungo wengi kuliko Yanga

Dakika ya 21 Mbao Fc wanapata Kona , Ni ya tatu katika mchezo wa leo

Inapigwa kona fupi na Said Junior anajaribu kumchungulia Kabwili lakini vipimo vinagoma

Dakika ya 22 Mpira wa Adhabu unapigwa na Haruna Moshi mpira unamkuta Tambwe lakini kichwa chake kinaenda nje ya Lango

Dakika ya 25 Mbao Fc wanacheza vizuri na Amosi Kadikilo anamimi krosi ambayo hata hivyo inaenda nje ya lango la Yanga

Dakika 30

Mbao Fc 0 – 0 Yanga

Dakika ya 31 Mbao wanapata Kona nyingine katika mchezo wa leo

Washabiki wa Yanga wanaonekana kutoridhishwa na maamuzi ya Refa

Dakika ya 33 Yanga wanafanya Shambulizi zuri lakini Makambo anakosa mpira wa Kichwa

Dakika ya 34 Yanga wanacheza Free Kick moja ya Kiufundi lakini kipa Metacha Mnata anaicheza

Dakika ya 35 Mbao wanapata Kona nyingine kichwa cha Pastory Athanas kinaenda nje ya Lango

Dakika ya 38 Haruna Moshi Shaaban anaonyeshwa kadi ya Njano

Dakika ya 40

Mbao 0 – 0 Yanga

Dakika ya 41 Amis Tambwe anawekewa pasi ya Kifua lakini shuti lake linapaa juu ya Lango la Mbao

Dakika ya 42 Yanga wanafanya Shambulizi zuri krosi ya Ajibu inashindwa kumfikia Makambo

Dakika ya 44 Mrisho Ngassa anamimina Krosi Ajib anapiga kichwa Kipa Metacha Mnata anaudaka mpira

Goaaaaaaal Ndaki Robert anaipatia Mbao Fc kwa kichwa krosi ya Amos Charles Kadikilo

Mbao 1 – 0 Yanga

HALF TIME

Mbao 1 – 0 Yanga

KIPINDI CHA PILI

Goaaaal dakika ya 49 Yanga wanasawazisha kupitia kwa Makambo

Yanga wanaamka sasa na wanapata Kona dakika ya 53

Dakika ya 55 Mrisho Ngassa anawakosa Mbao Fc Metacha anaokoa

Dakika ya 58 Yanga wanapata kona na almanusra wafunge bao

Dakika 65

Mbao Fc 1 – 1 Yanga

Dakika ya 66 Eric Murilo anapewa kadi ya njano kwa mchezo usio wa Kiungwana

Dakika ya 67 Yanga wanapata Penati baada ya mchezaji wa Mbao Fc kudaka mpira

Goaaaaaaal Amis Tambwe anafunga penati

Mbao 1 – 2 Yanga

Dakika ya 71 Yanga wanafanya mabadiliko ya Kumtoa Amis Tambwe na nafasi yake inachukuliwa na Andrew Vincent

Dakika ya 72 Yanga wanapata kona

Dakika ya 73 Yanga wanawakosa kosa Mbao Fc

Dakika ya 75 Deus Kaseke anaingia KUCHUKUA nafasi ya Ibrahim Ajibu

Dakika ya 80

Mbao Fc 1 – 2 Yanga

Dakika ya 82 Ngassa anatoka anaingia Mo Banka

Dakika 4 za Nyongeza kabla ya Mechi Kumalizika

FULL TIME

Mbao 1 – 2 Yanga ( Ndaki Robert, – Makambo, Tambwe )

Install App Bora Ya Michezo Hapa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY