Mrisho Ngassa amjibu Jerry Muro kisomi

Mrisho Ngassa amjibu Jerry Muro kisomi

0

Mrisho Ngassa amjibu Jerry Muro kisomi

Siku moja baada ya aliyekuwa afisa habari wa Yanga Jerry Muro kuwa wachezaji Mrisho Ngassa na Haruna Moshi wachezaji wa Yanga hawa kuwa muda ushawapita na hawastahili kucheza Yanga kwasasa Mrisho Ngassa ameibuka na Kumjibu kisomi Jerry.

Jerry katika maelezo yake alisema

“Ifikie hatua klabu iangalia wachezaji ambao wanaleta hamasa ndani ya timu, vema ikasajili ambao wanaweza kupambana kwa ari na nguvu zote, ukimtazama Ngassa na Boban hawa muda wao umeshaisha na ni vema wakafanya mambo mengine nje ya soka”

Naye Mrisho Ngassa amekuja akamjibu kisomi na Kiheshima lakini akibakiza ukweli kuwa kama wao wangekuwa wabovu kiasi hiko basi timu isingekuwa ikiongoza Ligi.

“Kwetu tumefundishwa mkubwa hakosei, kwahiyo mimi siwezi kumlaumu yeye kajaliwa kipaji cha Kuongea mimi nimejaaliwa kipaji cha kucheza mpira “

Aliendelea kusema Ngassa

” Kama sisi wabaya sasahivi timu inaongoza ligi sisi tungekuwa wabaya timu ingekuwa nafasi ya 10 “

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY