Msiogope : Hao Al Ahly wanamajeruhi 9

Msiogope : Hao Al Ahly wanamajeruhi 9

0

Alexandria, Misri
KIKOSI cha Simba cha Tanzania kitakwaana na Al Ahly ya Misri kesho Jumamosi katika mji wa Alexandria nchini humo na habari njema kwa Wekundu wa Msimbazi hao wanaonolewa na Mbelgiji Patrick Aussems ni kwamba wapinzani wao watawakosa wachezaji tisa kwa sababu ya majeruhi.


Taarifa kutoka Misri zinasema nyota watakaokosekana wote ni tegemeo ambao ni nahodha wao Hossam Ashour, washambuliaji Walid Azarou na Marawan Mohsen, wakongwe Ahmed Fathy, Walid Soliman na beki Mohamed Naguib hawatatia miguu uwanjani kutokana na majeruhi.
Nyota wapya Ramadan Sobhi, Yasser Ibrahim na Hamdy Fathy nao pia wanachechemea kutokana na maumivu kwa hiyo hawatakuwepo uwanjani.

Install App bora ya Michezo Tanzania


Kocha wa Al Ahly raia wa Uruguay Martin Lasarte ameweka wazi kwamba kukosekana kwa wachezaji hao ni pigo kwake.


“Tunaendelea vizuri na mazoezi lakini tatizo letu ni kwamba tumekuwa tukicheza mechi kila baada ya masaa 72, jambo hilo limekuwa likiwachosha wachezaji huku wengine wakiumia,”alisema Lasarte.
“Jambo hili si sahihi kabisa, kukosekana kwa mastaa hao kunamaanisha kwamba mechi itakuwa ngumu.”


Vinara hao wa Kundi D, wamekuwa wakicheza mechi mara kwa mara kukimbizana na kasi ya Ligi Kuu Misri.
Hata hivyo vyombo vya habari vya Misri vimekuwa vikilaumu jopo la madaktari wa klabu, kutokana na majeruhi hayo.
Lakini kurudi kwa kiungo Salah Mohsen ni habari njema kwa Lasarte, ambaye kikosi chake hakijapoteza mechi katika kundi hili, waliwafunga AS Vita katika mechi ya ufunguzi kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 na JS Saoura ya Algeria.


Simba wao wanaenda kwenye mechi wakiwa na historia ya kichapo cha mabao 5-0, kutoka AS Vita ya DRC, lakini katika mechi ya awali waliichapa JS Saoura 3-0 nyumbani.

Install App bora ya Michezo Tanzania

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY