Mtazamo wa Julio uwezo kati ya Kapombe na Zana Coulibaly

Mtazamo wa Julio uwezo kati ya Kapombe na Zana Coulibaly

0

Mtazamo wa Julio uwezo kati ya Kapombe na Zana Coulibaly

KOCHA wa Dodoma FC, inayopambania kucheza ligi kuu msimu ujao, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amesema licha ya uwezo wa Mbukinafaso, Zana Coulibaly ambao ameonyesha hivi karibuni, lakini hawezi kumfunika Shomary Kapombe.

Kapombe yupo nje ya uwanja kwa miezi kadhaa sasa akiuguza majeraha ya mguu aliyopata wakati akitumikia Taifa Stars, ambapo klabu yake ya Simba ilichukua jukumu la kumsajili Zana aje kuwa mbadala wake kwa kipindi hiki ambacho yuko majeruhi.

Kagere akataa Tuzo Simba

Zana ameonesha uwezo wa hali ya juu kwenye mechi kubwa mbili alizocheza hivi karibuni, akiisaidia timu hiyo kupata ushindi kwenye michezo mitatu mfululizo dhidi ya Mwadui, Yanga na Al Ahly ya Misri.

Akizungumza nasi Julio alisema kuwa, watu wasimfananishe Kapombe na Zana kwani watakuwa wanamnyima haki ya msingi mchezaji huyo.

“Nchi mzima inamjua Kapombe ni mchezaji wa aina gani, kwa hiyo mnapoamua kumfananisha na mchezaji mwingine muwe na pointi za kutosha.

“Yule Kapombe atakupa vitu vingi kwa wakati mmoja, atakaba, atafunga, atapiga krosi na atafanya kila kitu uwanjani.Huyo Zana mwambieni atafute namba nyingine akacheze siku Kapombe atakaporejea,” alisema Julio.

Install App Bora Ya Michezo Hapa

source : Champion

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY