Ratiba ligi kuu TPL 6 February 2019

Ratiba ligi kuu TPL 6 February 2019

0

Ratiba ligi kuu TPL 6 February 2019

Ligi kuu soka ya Tanzania bara Itaendelea 6 February 2019 kwa mechi 6 kuchezwa katika Viwanja mbalimbali nchini Tanzania.

Singida United wataikaribisha Yanga ambao ndiyo vinara wa ligi kuu soka ya Tanzania bara, Mechi ikichezwa katika uwanja wa NAMFUA mkoani Singida.

JKT Tanzania watakuwa nyumbani uwanja wa Isamuhyo Mbweni jijini Dar Es Salaam kucheza na Biashara United kutoka mkoani Mara.

Azam waendelea na mazoezi kuikabili Alliance TPL

Tanzania Prisons wanaopambana kutoka mkiani mwa Ligi kuu wakiwa nafasi ya 18 watakuwa nyumbani uwanja wa Sokoine kuwakaribisha vijana kutoka wilaya ya Ilemela jijini Mwanza Mbao Fc.

Stand United chama la wana wapiga debe kutoka manispaa ya Shinyanga watakuwa wenyeji wa Ndanda Fc kutoka Mtwara.

Wakubwa Wanafaidi – Install App Ujionee

Nao wajukuu wa Mtwa Mkwawa vijana wa Lipuli kutoka Iringa msomaji wa Kwataunit.co.ke watakuwa nyumbani Uwanja wa Samora kuwakaribisha watoto wa Kinondoni KMC ya jijini Dar Es Salaam.

Na mechi ya Mwisho kwa siku ya 6 February 2019 itazikutanisha Azam Fc dhidi ya Alliance mechi itakayochezwa saa mbili kamili usiku uwanja wa Azam.

Install App bora ya Michezo Tanzania

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY