Simba: Aliyewakazia Al Ahly hatihati kuikosa Yanga

Simba: Aliyewakazia Al Ahly hatihati kuikosa Yanga

0

Aliyewakazia Al Ahly hatihati kuikosa Yanga

Wakati Simba ikijipanga vyema kuwakabili Yanga katika mchezo wa kesho utakaochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam kuna hofu imetanda kwa washabiki wa Simba.

Hofu hiyo inatokana na beki kisiki Juuko Murshid ambaye aliwakazia vilivyo waarabu wa Al Ahly katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika jijini Dar Es Salaam.

Juuko katika mazoezi ya jana yaliyokuwa yakifanyika jana katika uwanja wa Boko Veteran alishindwa kujumuika na wenzake katika mazoezi ya pamoja huku akifanya mazoezi ya baiskeli akiwa nje ya uwanja.

Muda wowote Simba itamtangaza kocha huyu mpya

Katika mazoezi ya jana alikuwa akifanya mazoezi ya baiskeli ambayo ilipelekwa uwanjani kwaajili ya mazoezi ya wachezaji ambao hali zao si nzuri sana kiafya ambapo alikuwa akifanya na Asante Kwasi

Kocha wa Simba msomaji wa Kwataunit.co.ke Mbelgiji Patrick Aussems alifunguka kuwa Juuko alipata maumivu kwenye mchezo wa Al Ahly lakini bado haijafahamika moja kwa moja kama atacheza katika mchezo wa kesho .

Katika Mchezo kati ya Simba na Al Ahly Juuko alikuwa mwiba mchungu kwa washambuliaji wa Al Ahly kutokana na kuwatibulia kila mpango waliokuwa wakiufanya

Install App bora ya Michezo – Michezo Plus App

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY