Usajili Yanga: Kipa huyu anatua Yanga

Usajili Yanga: Kipa huyu anatua Yanga

0

Usajili Yanga: Kipa huyu anatua Yanga

BAADA ya kushindwa kumnasa kipa wa Tanzania Prisons, Aaron Kalambo, katika usajili wa dirisha dogo, Klabu ya Yanga huenda ikafanikisha mpango huo msimu ujao, kwani tayari mlinda mlango huyo amesema anajiandaa kukipiga kwenye timu hiyo.

Msimamo ligi kuu Tanzania Bara TPL 2018/2019

Katika usajili wa dirisha dogo, Yanga walishafikia hatua za mwisho kumnasa ili achukue nafasi ya Beno Kakolanya anayewasumbua lakini wakakwama.

Prisons waliigomea Yanga wakidai hawawezi kumwachia kipa wao huyo  kutokana na timu yao kuwa katika hali mbaya kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Kalambo akiwa ni  tegemeo.

App kwaajili ya Wakubwa 18 + Wakubwa Wanafaidi

Akizungumza nasi, Kalambo alisema hivi sasa anaipigania Prisons isishuke daraja, lakini baada ya hapo mabosi wake watakuwa wamejipanga kumpata mrithi wake ili yeye akakipige Jangwani.

“Ningelazimisha kuondoka wakati wa usajili wa dirisha dogo isingekuwa ni uungwana kutokana na timu yangu kushika mkia kwenye ligi, kwa sasa nataka niibakize Ligi Kuu na baada ya hapo nitakuwa sina kizuizi.

“Viongozi wangu hawana tatizo, kipindi kile mimi mwenyewe niliona si sahihi kuondoka, lakini Ligi Kuu ikimalizika na Prisons kubaki msimu ujao, sitakuwa na kuzuizi labda kama tutashindwana katika masuala ya mkataba,” alisema Kalambo.

Install Michezo Plus App

source : Bingwa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY