Zahera agundua gonjwa jipya Yanga

Zahera agundua gonjwa jipya Yanga

0

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amebaini kuwa wachezaji wake wamekuwa wakichoka haraka na kushindwa kuonyesha kiwango kizuri katika mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga juzi walibanwa na Singida United na kutoka nao suluhu katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Namfua, mjini Singida.

Hiyo ni sare ya pili kwa Wanajangwani hao ambao katika mchezo uliopita, waliambulia pointi moja kutoka kwa Coastal Union ya Tanga, timu hizo zilipofungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Akizungumza nasi jana, Zahera alisema katika mchezo huo wa juzi, nyota wake walionekana kuchoka na kushindwa kufanya kile ambacho walikitarajia.

Install Michezo Plus App

“Katika mechi tulizocheza za hivi karibuni, wachezaji wangu wameshindwa kufanya kile ambacho nawaelekeza. Mfano ukimwangalia Matheo Antony na Haritier Makambo, wamekuwa hawapo makini kabisa pale wanapofika katika eneo hatari.

“Hii imeonekana tangu kwenye michezo ya nyuma, lakini imeendelea na katika mchezo huu dhidi ya Singida United. Makambo tangu arudi kutoka Congo (DRC), kiwango chake kimebadilika sana,” alisema.

Akizungumzia kikosi chake kwa ujumla, Zahera alisema wachezaji wanaonekana kuchoka na ndiyo maana katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union, aliwahi kumtoa Ibrahim Ajib, kwani alionekana kutoka mchezoni.

“Juzi pia sikuweza kumchezesha Haruna Moshi, kwani nilikuwa nataka kumpumzisha, ukiangalia bado tuna mechi ya ugenini dhidi ya JKT Tanzania, Tanga,” alisema.

Kikosi hicho kiliondoka jana kutoka Singida kuelekea Tanga kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya JKT Tanzania, unaotarajiwa kuchezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Yanga wameendelea kushika usukani katika msimamo wa ligi, wakijikusanyia pointi 55 kati ya mechi 22 walizocheza, wakishinda 17 na kutoa sare nne, huku wakipoteza mmoja.

App kwaajili ya Wakubwa 18 + Wakubwa Wanafaidi

source : Bingwa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY