Zahera anaondoka Yanga mwisho wa Msimu ataja sababu

Zahera anaondoka Yanga mwisho wa Msimu ataja sababu

0

Zahera anaondoka Yanga mwisho wa Msimu ataja sababu

KOCHA Mkuu wa Klabu ya Yanga Mwinyi Zahera amesema, ataachana na timu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania kama ataendelea kukosa ushirikiano kutoka kwa wanachama hususani kwenye suala la michango ya kuisaidia timu.

Akizungumza na mwandishi wa nasi hii leo Zahera amesema, wamekuwa wakiwasihi wanachama kuhusu suala zima la kuisaidia timu bila mafanikio na kwamba wamefanya matangazo wiki ya nne sasa kwa ajili ya kuichangia timu lakini mwitikio ni mdogo mno ukilinganisha na idadi yao.

“Kama mambo yataendelea hivi basi msimu huu ukimalizika nitaachana na Yanga kwasababu tayari nimeshafanya mengi sana kwa ajili ya timu, naamini hakuna mtu atachukia kwa maamuzi yangu. Nimewasaidia kwa vitu vingi ila naona kama vile wao wenyewe hawapendi kujisaidia, wanachama na mashabiki wa Yanga Tanzania wakumbuke ule msemo UKIJISAIDIA NA MUNGU ATAKUSAIDIA, ”.

Install App Bora Ya Michezo Hapa

“Tuliwaambia wanachama na mashabiki tuijenge timu sisi wenyewe ila hakuna chochote kilichofanyika, mpaka sasa imepatikana sh 25 milioni tu, binafsi niliweka Milioni mbili na mimi si shabiki wala mwanachama. Yanga ina wanachama matajiri wengi sana ila nashindwa kuelewa kwanini hawachangii, kama kila tajiri angetoa milioni mbili tungeweza hata kununua wachezaji wazuri ifikapo Mei, ” amesema.

Zahera amemaliza kwa kuwataka viongozi, wanachama na mashabiki waache kusema tu wanaumia timu ikifanya vibaya, badala yake waisaidie ifanye vizuri na kama hawataki basi wajue kwa upande wake itakuwa ngumu sana kuendelea kujitolea kwa watu ambao hawajali.

source : Boiplus.co.tz

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY