Zahera : Tuna Uhakika wa kushinda

Zahera : Tuna Uhakika wa kushinda

0

Zahera : Tuna Uhakika wa kushinda

Kocha wa Klabu ya Yanga Mcongo Zahera Mwinyi amewaaminisha washabiki wa Yanga kuwa amefanya marekebisho yote yaliyokuwa yakiisumbua Yanga na kuahidi kushinda mchezo wa leo.

Zahera alisema wazi kuwa watu wataishangaa Yanga itakayocheza na wasitegemee kuona Yanga ile iliyocheza na Simba mzunguko wa Kwanza.

“Sisi tutaenda kucheza bila hofu yoyote, mashabiki wetu waje bila hofu, tumejiandaa na tunaamini tuna asilimia zote za kupata ushindi.“Kikosi changu kimesharekebisha madhaifu yake yote na hatutarudia yale yaliyotugharimu katika michezo yetu iliyopita. Yanga itakayocheza kesho (leo) ni mpya, mashabiki waje uwanjani tuna uhakika wa kushinda,” alisema.

Install App bora ya Michezo – Michezo Plus App

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY