As vita waingilia ugomvi wa Simba na Mazembe

As vita waingilia ugomvi wa Simba na Mazembe

0

DAKTARI wa AS Vita Club, Nowa Lelo amefunguka kuwa amefurahishwa na hatua ya Simba kupangwa na TP Mazembe kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Lelo alitua Tanzania wiki iliyopita na kushuhudia timu yake ikitupwa nje na Simba kwa mabao 2-1, huku Simba ikidondoka mdomoni mwa mabingwa wa zamani wa michuano hiyo ya Afrika.

Akizungumza nasi , Lelo alisema amefurahi kuona Simba ikitupwa kwa wapinzani wao, TP Mazembe, kwa kuwa anafahamu hawataweza kuchomoka kwa Wakongo hao na kwa upande fulani watakuwa wamelipiwa kisasi cha kuondoshwa mashindanoni.

“Nilikuwa naomba Simba ipangwe na TP Mazembe na kweli imekuwa hivyo, nafikiri sasa mwisho wao utakuwa umefika, hawataweza kupata ushindi kwa Mazembe hata iweje, kwa hiyo kwa upande fulani tutakuwa tumelipiwa kisasi,” alisema Lelo.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY