As Vita wala hawahofii jambo hili kwa Simba

As Vita wala hawahofii jambo hili kwa Simba

0

As Vita wala hawahofii jambo hili kwa Simba

Kocha msaidizi wa klabu ya AS Vita, Roul Shungu amesema wanafahamu Simba wana tabia ya kujaza uwanja wakiwa nyumbani lakini jambo hilo haliwatishi kuelekea mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika utakaopigwa keshokutwa Jumamosi.

Vita watakuwa wageni wa Wekundu hao ambao wameubatiza mchezo huo jina la ‘Do or Die’ (kufa au kupona) kwakua endapo watashinda watatinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo na wakifungwa safari yao itakuwa imeishia hapo.

Shungu ambaye aliwahi kuifundisha Yanga miaka ya nyuma amesema Simba ni timu bora na ina mashabiki wengi ambao hujitokeza kwa wingi uwanjani lakini jambo hilo haliwezi kuwafanya kushindwa kupata matokeo ya ushindi. “Ni kweli Simba ina mashabiki wengi na wanaweza kujaza uwanja siku hiyo lakini sisi hatutishiki juu ya hilo, tunachojua timu bora hushinda uwanjani kutokana na maandalizi iliyofanya,” alisema Shungu.

Licha na kukiri kuwa Simba ni bora kwa sasa lakini Shungu anaamini timu yake ya Vita ina nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo na kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

credit : SDF Sports

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY