As Vita wazuiwa uwanja wa Taifa

As Vita wazuiwa uwanja wa Taifa

0

Wakati joto la mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na AS Vita likizidi kupanda, wageni hao wamejikuta kwenye mzozo mkubwa wakati wakijiandaa kufanya mazoezi yao ya mwisho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Leo jioni msafara wa AS Vita ulizuiwa kwa muda kuingia Uwanja wa Taifa na kundi la watu wanaodaiwa ni makomandoo wa Simba kwa madai kuwa, kwenye basi walilokuwa wakilitumia alikuwemo Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera. Hata hivyo, vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 zilizimwa baada ya kutoonekana kwa Zahera kama ilivyokuwa ikidaiwa na makomandoo hao.

As Vita waliingia uwanjani hapo wakiwa na magari mawili, likiwemo basi la Simba ambalo limetolewa kwa wageni hao lakini, katika kile kinachoelezwa kukwepa hujuma, basi hilo liliingia likiwa na watu sita tu ambao, ni viongozi. Kisha likawepo basi dogo ambalo ndilo lilitumika kuwabeba wachezaji wa AS Vita.

source : Mwanaspoti

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY