As vita yafichua usajili Yanga

As vita yafichua usajili Yanga

0

As vita yafichua usajili Yanga

YANGA inafanya mambo yao kwa usiri wakijipanga taratibu juu ya kikosi chao cha msimu ujao lakini siri imefichuka wamefanya mazungumzo ya ana kwa ana na mastaa watatu wa AS Vita ya DR Congo.

Iko hivi! wakati AS Vita ikiwa hapa nchini kisha kuchapwa mabao 2-1 dhidi ya Simba kuna kigogo mmoja alitua kwa siri kwenye hoteli yao kisha kufanya kikao na mastaa hao. Akiwa katika hoteli hiyo mmoja wa mabosi wa ufundi wa AS Vita amefichua kigogo huyo aliteta na winga wa timu hiyo Tuisila Kisinda ambaye katika mchezo huo hakuwa kwenye kiwango bora kama mechi za nyuma.

Kasi ya Kisinga ndiyo iliyowavuta Yanga na bado inaonyesha nia ya kumwania kwani inasaka mtu anayejua kukimbiza. Mbali na Kisinda pia kigogo huyo ambaye alikuwa na mchango mkubwa kifedha katika usajili uliopita kujenga kikosi chao cha sasa alikutana na mfumania nyavu namba moja wa timu hiyo Makusu Mundele. Yanga inamhitaji Mundele wakipambana na klabu moja ya Morocco na Simba zote zikihitaji huduma ya mshambuliaji huyo.

Hata hivyo, kigogo huyo (jina tunalo) wamekubaliana na Mundele wakutane DR Congo wiki chache mbele wakikutana pamoja na meneja wa mshambuliaji huyo. Pia bosi huyo alikutana tena na beki wa kati Yannick Bangala ambaye ni nahodha wa kikosi cha Chan kwa DR Congo.

Bangala ambaye ni kiraka pia anamudu kucheza nafasi zingine tatu katika safu ya ulinzi na mechi mbili dhidi ya Simba alicheza nafasi mbili tofauti. Wakati Simba ikiwa ugenini jijini Kinshasa, Bangala licheza kama beki wa kulia lakini mchezo baina ya timu hizo wikiendi iliyopita alicheza beki wa kati nafasi ambayo anaitumikia akiwa na kikosi cha Chan DR Congo.

Aliyefichua habari hiyo ni kocha msaidizi wa AS Vita, Roul Shungu ambaye alifafanua juu ya kikao hicho huku bosi huyo akimpa kazi nyingine kocha huyo. Shungu alisema kigogo huyo wa Yanga licha ya kuonyesaha kuwahitaji mastaa wao hao pia amemtaka kumtafutia straika hatari zaidi endapo watamkosa Mundele.

“Nikweli huyo kiongozi (anamtaja) alikuja pale hotelini alipomaliza kutusalimia aliomba ruhusa ya kuongea na hao wachezaji,” alifafanua Shungu.

source : Mwanaspoti

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY