Clatous Chama mtu hatari sana

Clatous Chama mtu hatari sana

0

CLATOUS Chama wa Simba ameitikisa Afrika kwa kutupia mabao ya usiku na muhimu kwa timu yake katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Chama aliyesajiliwa na Simba msimu huu, ameonekana kuwa mchezaji muhimu kwa kufunga mabao hayo yanayoifanya mpaka sasa Simba kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

Ikumbukwe kuwa, Simba ilipata tiketi ya kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 ambapo cheche za Chama zilianza kuonekana kwenye mchezo wao wa kwanza wa hatua ya awali dhidi ya Mbabane Swallows ya Eswatin kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Kwenye mchezo huo, Simba ilishinda mabao 4-1 ambapo Chama alifunga bao la nne dakika ya 90 akimalizia pasi ya Hassan Dilunga.

Pia kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa nchini Eswatin, Chama alifunga mabao mawili dakika ya 27, 31 na alitoa pasi ya bao kwa Meddie Kagere dakika ya 62 kwenye ushindi wa mabao 4-0.

Katika mchezo wa mtoano dhidi ya Nkana FC, Chama alitoa pasi ya bao lililofungwa na Mkude dakika ya 29, bao la tatu ambalo lilikuwa la ushindi alifunga dakika ya 88 akimalizia pasi ya Hassan Dilunga kwenye ushindi wa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa.

Hatua ya makundi mchezo wao wa kwanza dhidi ya JS Saoura, Uwanja wa Taifa, Chama alitoa pasi ya bao lililofungwa na Okwi dakika ya 45 kwenye ushindi wa mabao 3-0.

Alimaliza kuonyesha thamani ya uwepo wa mashabiki juzi dhidi ya AS Vita, Chama aliipeleka tena Simba hatua ya robo fainali baada ya kufunga bao dakika ya 90.

Hivyo mpaka sasa Chama amefunga mabao matatu dakika za lala salama huku mawili yakiivusha Simba kwenye hatua muhimu, ametoa jumla ya pasi tau za mabao ndani ya Simba kimataifa akiwa na jumla ya mabao matano kwa sasa

credit :GPL

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY