Dalali: TP Mazembe watapigwa tu

Dalali: TP Mazembe watapigwa tu

0

MWENYEKITI wa zamani wa klabu ya Simba, Hassan Dalali, amesema ana matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na ubora wa kikosi chao.

Simba wanatarajiwa kucheza na TP Mazembe Aprili 5, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na baadaye kurudiana Aprili 12 mjini Lubumbashi.

Akizungumza nasi jijini jana,  Dalali alisema TP Mazembe watapigwa, kwani kikosi chao kinauwezo wa hali ya juu wa kusakata kabumbu.

Dalali alisema anaamini hakuna timu itakayotoka salama kwenye Uwanja wa Taifa, ikiwamo TP Mazembe kwa kuwa wamedhamiria kufika mbali katika michuano hiyo.

“Kawaida yetu tuna mipango mingi kabla ya mchezo, lakini kubwa ni mikutano ya mara kwa mara ya matawi ya kupeana majukumu,” alisema.

Wakati huo huo, mwanachama mwenye kadi namba 532 ya uanachama wa Simba, Abdallah Athumani, alisema wao ni kiboko ya watu wa DR Congo.

“Nina uhakika tunashinda, TP Mazembe hii si ya kipindi kile, wanafungika,” alisema.

Simba walifanikiwa kutinga robo fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AS Vita katika mchezo wa marudiano wa Kundi D, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY