Dismas Ten amwijia Juu Manara ishu ya Zahera,Akumbusha ya Masoud Djuma

Dismas Ten amwijia Juu Manara ishu ya Zahera,Akumbusha ya Masoud Djuma

0

Siku moja baada ya afisa habari wa Simba Haji Manara kulalamikia suala la kocha wa Yanga Zahera Mwinyi kuonekana kuwa karibu na wapinzani wao AS VITA Dismas Ten amekuja na kauli kuhusu tamko la Haji manara.

Dismas Ten kwanza amefunguka kuwa kama kuna chochote kibaya kitamkuta kocha wao basi uongozi wa Simba unahusika lakini pia amepost picha ya Masoud Djuma na Haruna Niyonzima ambao walienda kwenye kikosi cha Rayon Sports walipokuja Tanzania kucheza na Yanga.

Kauli za kichochezi dhidi ya kocha Zahera Mwinyi, wana Yanga wote tuamini kuwa jambo lolote baya litakalo mpata kocha wetu basi Uongozi wa Simba unahusika… ama la wajitokeze hadharani kukanusha au kuzikemea kauli hizo…! Soka ni mchezo wa kiungwana, vipi wengine waugeuze kuwa sehemu ya uchochezi na ubaguzi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY