Habari mpya kutoka Yanga usiku wa leo 14 March 2019

Habari mpya kutoka Yanga usiku wa leo 14 March 2019

0

Habari mpya kutoka Yanga usiku wa leo 14 March 2019

Kikosi cha Yanga leo kimefika salama mkoani Iringa ambapo Yanga imeifuata Lipuli kwaajili ya mchezo wa ligi kuu soka ya Tanzania bara TPL utakaochezwa jumamosi 16 March 2019.

Akizungumza kuelekea mchezo huo kaimu mwenyekiti wa klabu ya Yanga Samwel Lukumay ameeleza kuwa kikosi kimefika salama tayari kwa mchezo huo lakini pia leo hawatafanya mazoezi mpaka kesho.

KUHUSU MWANDILA KUACHIWA KIKOSI.

Samwel Lukumay ameelezea kuwa hawana wasiwasi na kocha msaidizi Noel Mwandila kwani amekuwa na timu ya Yanga kwa msimu wa tatu sasa kitu ambacho hawana wasiwasi naye

Mwandila ndiye atakayekuwa kwenye benchi Yanga ikiikabili Lipuli kwani kocha mkuu Zahera Mwinyi atakuwa nchini Congo kwa maandalizi ya timu ya Taifa.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY