Hii ndiyo rekodi Bocco anayoelekea kuivunja

Hii ndiyo rekodi Bocco anayoelekea kuivunja

0

Hii ndiyo rekodi Bocco anayoelekea kuivunja

MSHAMBULIAJI wa Simba na nahodha wa kikosi hicho, John Bocco ameonekana kuwa mwiba kwa mechi saba za mkoani kwa kufunga sita huku wakiwa wamesaliwa na mechi nane nje ya Dar.

Bocco kwa sasa amefunga jumla ya mabao tisa katika ligi hiyo akiwa sawa na mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe mwenye idadi hiyo ya mabao.

Msimu uliopita akiwa na kikosi hicho, mkoani aliweza kufunga jumla ya mabao saba kati ya 14 ambayo aliweza kufunga.

Katika msimu huo wa 2017-18 alifunga mkoani dhidi ya Prisons (0-1), Mwadui FC (2-2) moja, Kagera Sugar (01), hapa alifunga mabao mawili mawili kila mechi dhidi ya Njombe Mji (02) na Ndanda FC(0-2).

Simba hadi sasa kwenye Ligi Kuu Bara imefanikiwa kucheza mechi saba nje ya Dar ambazo ni dhidi ya Ndanda(0-0), Mbao (1-0), Mwadui (1-3), Stand United (0-2), JKT Tanzania (0-2), African Lyon (0-3) na Lipuli FC (1-3).

Katika mechi hizo saba Bocco amefanikiwa kufunga mabao sita kati yale tisa aliyofunga msimu huu. Bocco amefunga dhidi ya Lyon ambako amefunga mabao mawili, dhidi ya Stand United alifunga mawili na mchezo wa Mwadui alitupia mawili. Nyota huyo kwa sasa ana mabao hayo tisa katika mechi 20 ambazo Simba wamecheza

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY