Kikosi cha Simba dhidi ya As Vita leo 16 March 2019

Kikosi cha Simba dhidi ya As Vita leo 16 March 2019

0

Kikosi cha Simba dhidi ya As Vita leo 16 March 2019

Mbelgiji wa Simba Patrick Aussems ni kama ameshaonyesha kosi lake ambalo ataenda kulitumia Simba itakapokuwa ikiivaa As Vita leo majira ya saa moja usiku uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

Kuelekea mchezo huo kikosi cha Simba kikiwa katika mazoezi ya Mwisho Aussems ameonekana kuwapanga

Aishi Manula Golini, Zana Coulibaly na Mohammed Hussein Shavu la kulia na Kushoto.

Huku katika mabeki wa kati akiwapanga Paul Bukaba na Erasto Nyoni ambao walikuwa wakipishana kucheza na Pascal Wawa, Kwahiyo hapa Ni wazi Pascal wawa ataanza na mmoja kati ya hawa Bukaba na Erasto Nyoni.

Siri 4 alizotoa Zahera kuhusu Simba kwa As Vita

Napo katikati ambapo Simba ilizoea kuwaanzisha wachezaji watatu ambao ni Mkude, Kotei na Chama lakini safari hii Mkude akikosekana kutokana na kadi Aussems amewaanzisha James Kotei, Clatous Chama huku Hassan Dilunga na Mzamiru Yassin wakionekana kupishana mmoja akiwekwa na kisha mwingine tena anakuja kucheza nafasi yake.

Kwahiyo msomaji wa Kwataunit.co.ke Hapa wenye uhakika wa kuanza ni Clatous Chama, James Kotei huku mmoja kati ya Mzamiru na Dilunga anaweza kuanzia sub.

Mbele kama kawaida ule utatu wa Simba ndiyo ulionekana kuanza kwa pamoja ambapo John Bocco, Meddie Kagere na Mganda Emmanuel Okwi wakionekana kuanza pamoja.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY