Likipita hili Manji anarudi Yanga

Likipita hili Manji anarudi Yanga

0

Likipita hili Manji anarudi Yanga

Wakati wengi wakiwa na matumaini mengi kuwa ipo siku aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji atarudi huenda jambo hilo likafanikiwa kama mchingo huu utatiki na kukaa sawa.

Kwasasa Yanga walikuwa kwenye mpango wa kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi za baadhi ya viongozi wa kamati ya utendaji waliojiuzulu, kamaimu mwenyekiti na mwenyekiti wa klabu hiyo.

Lakini zoezi hilo limekuwa likikubwa na changamoto nyingi zinazokwamisha zoezi hilo kufanyika.

Moja kati ya viongozi wa kamati ya utendaji ambao wamesalia Samwel Lukumay ambaye pia ni kaimu mwenyekiti wa klabu kwasasa amefunguka kuwa wameomba mkutano mkuu wa dharura wa wanachama.

Sababu kuu ya kuomba mkutano mkuu wa dharula wa wanachama ni kuwaomba wanachama waruhusu kufanya uchaguzi wa viongozi wote yani ufanyike uchaguzi mkuu na siyo uchaguzi wa wa kujaza nafasi chache pekee.

Sababu kubwa ya kufanya hivyo msomaji wa Kwataunit ni sababu mwakani kuna uchaguzi mkuu wa nchi hivyo wameonelea mambo yote ni vyema yafanyike mwaka huu hata uchaguzi huo unaopangwa kufanyika sasa wafanye wa jumla.

Hivyo basi kama ombi hilola kufanya mkutano wa dharula litatiki aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji huenda akarejea katika nafasi yake kwani huenda akagombea katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti na mambo yakaendelea kama Zamani Yanga ambayo haikuwahi kuwa na shida ndogondogo kipindi chake.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY