Mashine tegemeo yarejea mazoezini Simba

Mashine tegemeo yarejea mazoezini Simba

0

WACHEZAJI wa Simba, Haruna Niyonzima na Erasto Nyoni wamesema Jumamosi ni kufa au kupona dhidi ya AS Vita. Lakini habari njema ni kwamba straika matata wa Simba, Emmanuel Okwi jana jumatano jioni alirejea mazoezini kwenye uwanja wa Boko Veterani na wenzie. Simba inahitaji ushindi ili kufi kisha pointi tisa na kufuzu robo fainali Afrika.

Akizungumza nasi Niyonzima amesema kuwa, Simba inayo nafasi ya wazi kabisa na hawana mchecheto.

“Kikubwa ni kujituma ili kufanya vizuri katika mchezo wetu wa AS Vita ili kutinga hatua ya robo fainali ukiangalia katika kundi letu timu hazijapishana sana kimsimamo hivyo nafasi hiyo ipo kikubwa watu wanatakiwa waamini kuwa tunaweza.

“Simba ina kikosi kipana hata kama kuna wachezaji majeruhi mwalimu anajua jinsi ya kukipanga kikosi,” alisema Niyonzima ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga. Beki Erasto Nyoni ambaye anatokea kwenye majeruhi amesema; “Hatupaswi kukata tamaa, kwani bado tuna nafasi na kwa uwezo wake mola tutatumia vyema uwanja wa nyumbani kuhakikisha tunapata pointi tatu ambazo zitatupeleka robo fainali.

“Tumepoteza mchezo wetu dhidi ya Saoura lakini sio mwisho wa safari ya kuelekea robo fainali, kwani tuna nafasi kubwa tu iwapo tutatumia vyema uwanja wetu huu kwa kuwafunga AS Vita  kwani tukishinda mechi hiyo moja kwa moja tutakuwa tumefuzu kwenda hatua ya robo fainali.

“Kundi hili ni gumu hasa pale timu yeyote inapokwenda kucheza  uwanja wa ugenini mara nyingi huwa haipati matokeo chanya ila ikiwa nyumbani inafanya vizuri hivyo na sisi tutaitumia nafasi hii,” alisema Nyoni ambaye amewahi kucheza soka Burundi.

Spoti Xtra

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY